Filamu ilianza vyema. Masteringi wawili walioneshwa wakipania kucheza filamu ya kusisimua. Wakaanza kwa ziara za kushtukiza zisizo na giza. Wakaibuka na hata orodha ya mambo ya forodha. Mkaratasi usio na wasiwasi ukiwa na idadi ya vyenye ukakasi ukaoneshwa.
Wapo waliosimamishwa. Wapo waliopoteza kazi. Wapo waliokamatwa na kushtakiwa. Wapo waliopanda vyeo. Wapo walioshushwa vyeo. Wapo waliotakiwa kulipa kwa siku kadhaa. Wapo wasioonwa na kubaki wakinona.
Makontena yakaongezeka kupotea. Masteringi wakapania zaidi. Ikasemwa kuwa sasa idadi ni ya kutisha. Maelfu ya makontena yakasemwa yamepotea au hayakulipiwa kodi. Masteringi wakapania. Wakaungwa mkono. Wakaaminiwa.
Halafu,ukimya ukatawala. Kwa yale ya mwanzo na hata ya mwisho. Ni kama Masteringi kumalizia filamu vibaya. Ni kama filamu kuisha kwa maadui kushangilia ushindi na Masteringi kutoonekana tena. Filamu ilikuwa tamu na ya kutia hamu. Ilichezwa kiufundi bila kumwaga damu. Mwisho wake umeharibu. Tuendelee kuamini?
Christmas njema!
By Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam/JF
Hujui usemalo...sa ndo nini
ReplyDeleteMijitu mingine bwana kama we we uelewi hiyo filamu labla sababu lugha iliyotumika ni kizungu na kizungu kwako ni mama mkwe kwahiyo usitusemee watazamaji wengine wengi tunaelewa nini kinaendelea.kaa kimya acha wanaoelewa lugha waongee watakuhadithia baadae. Mungu mbariki Magufuli.
ReplyDeletefilamu bado haijaisha isipokuwa, wasanii wapo mapumziko mafupi wanajiandaa kwa part2, usiwe na haraka ndugu mtazamaji wasanii wengine wameshaongezwa na wameingia location tayari kwa ajili ya kuigiza ligame la kushtukiza.
ReplyDelete