Ni wazi kwamba CHADEMA ilianzishwa ili kuwa tofauti na CCM na vyama vingine. Tofauti hii lazima iwe dhahiri na ya kivitendo. CHADEMA iendeshwe kama vyama vya wenzetu kule Ulaya. Chama kikifanya vibaya ktk chaguzi kiongozi anawajibika. Uwajibikaji wa jumla " collective accountability".
Baada ya uchaguzi na michakato yake yote kukamilika chadema imepata nafasi ya pili, huku ikipata wabunge na madiwani kiduchu sana ukilinganisha na harakati, matarajio na nguvu iliyotumika.
Sasa nilitarajia na bado ninatarajia kuona vikao vya tathmini vikikaa na kufanya upembuzi wa kina kubaini sababu ya kushindwa kwenda ikulu na kuambulia wabunge na madiwani kidogo kiasi hiki.
Ni dhahiri kuwa kuna uzembe wa kupanga mikakati ya kupata ushindi mnono uliofanywa na viongozi wa ngazi zote. Hapa ndipo Kamanda Mbowe anabeba gunia la lawama kama kiongozi wa juu wa chama.
Alikuja na mbinu ya kubadili gia angani sawa Lakini je, mbinu hii ya kubadili gia angani imeleta athari gani chanya na hasi kwenye chama? Ukiziweka kwenye mizania athari hizi chanya na hasi, zipi zina uzito kuliko nyingine? Chama bado kina kasi ya kupendwa ama sasa kimefifishwa na mbinu ya kubadili gia angani?
Watu wengi huko mitaani wanaona CHADEMA ina wenyewe, na wenyewe ni akina Mbowe waliokaa Kitako wakamkaribisha Lowassa kisha mkutano mkuu ukaitishwa kama bosheni tu kuja "kuthibitisha" kilichoamriwa na "wakubwa".
Hii imepunguza ari ya kuibeba CHADEMA moyoni kama mwanzo. Maana wameona mpambanaji mwenzao Dr. Slaa aliyeumia ktk harakati za kukijenga chama na mkewe aliyevuja damu walivyopuuzwa na kutoswa kwa udhalili. Hii INA madhara makubwa kwa chama.
Sasa kamanda Mbowe jiuzuru ili aje mwingine na timu yake wafanye mikakati mipya ya kurudisha misingi ya chadema. Ikibidi hata kwa kuwafukuza waliokuja kufifisha nuru ya chama.
Aingie mtumbua majipu ndani ya chadema asafishe na kujenga matumaini mapya kwa wanachama. Vinginevyo chama kimekwama kwenye tope.
Wazohuru Toka Kwa G4N/Jamii Forums
Ushauri kwa CHADEMA: Tumeshindwa Uchaguzi, Mbowe Beba Mzigo
2
December 24, 2015
Tags
Koma wewe tumeibiwa kura
ReplyDeleteWewe kwanini ukuiba?acha sababu hafifu, mwandishi alichoshauri ni sahihi, bora kujiudhuru wakati unapendwa badala ya kinyume chake. Inaonekana watu wansubiria wang'olewe.
ReplyDelete