WABUNGE wanne wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wametajwa kukataa uteuzi wa nafasi ya uwaziri ili kujaza nafasi za wizara nne zilizokuwa wazi.
Hatua hiyo imetokana na kile kilichoelezwa kuwa ni hofu ya wabunge hao kushindwa kwenda na kasi ya Rais Dk. John Magufuli, ambaye aliwaapisha mawaziri wapya Desemba 12, mwaka huu.
Kwa mujibu wa gazeti la Mtanzania, wabunge wamedai kuwa kasi ya Rais Magufuli inawatia hofu.
“Kasi ya Rais Dk. John Magufuli ni nzito na kwangu ni ngumu na nilifikiri niko mimi peke yangu kumbe baada ya taarifa hizi nasikia na wenzangu wawili nao walikataa uteuzi.
“Niliarifiwa juu ya uteuzi lakini baada ya kupima nikaona hapana siwezi kazi ya uwaziri, bora ni baki na ubunge wangu,” alisema mbunge huyo ambaye hakutaka jina lake litajwe.
Wizara 4 zilizokosa Mawaziri
Wakati akitangaza Baraza la Mawaziri, Desemba 10, mwaka huu, Rais Magufuli alisema kuna baadhi ya wizara hazina mawaziri kutokana na sababu mbalimbali ikiwamo unyeti wa wizara hizo na kwamba anaendelea kuwatafuta.
Kutokana na hali hiyo Rais Magufuli aliteua manaibu waziri wa wizara hizo, huku akitoa ahadi kuwa atawatangaza mawaziri wake baadaye atakapomaliza mchakato.
Wizara hizo ni pamoja na Ujenzi, Uchukuzi na Miundombinu ambayo naibu wake ni Mhandisi Edwin Ngonyani na Wizara ya Fedha na Mipango, ambayo naibu wake ni Dk. Ashatu Kijaji.
Wizara nyingine ni Maliasili na Utalii, ambayo naibu wake ni Mhandisi Ramo Makani, Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi ambayo naibu wake ni Mbunge wa Jimbo la Nyasa mkoani Ruvuma, Stella Manyanya.
Kinana atoboa siri
Mwishoni mwa wiki akiwa mkoani Arusha, Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana, alitoa siri ya wabunge wanne ambao walipigiwa simu za uteuzi wa uwaziri, lakini walikataa kwa hofu ya kushindwa kwenda na kasi ya Rais Magufuli.
Alisema anachoamini ni kwamba Rais John Magufuli, atakuwa aliwaeleza baadhi ya wabunge kuhusu nia yake ya kuwateua katika nafasi hizo, lakini wao wakamwomba asiwape majukumu hayo kwa kuwa hawana uhakika wa kwenda na kasi anayohitaji katika Serikali yake.
Kinana alisema kinachojitokeza sasa ni kama alivyoshauri Rais Magufuli kuwa si vema kwa waziri aliyeteuliwa kufanya sherehe nyumbani kwake na kuita marafiki kwa kuwa wana mzigo mzito katika kuwatumikia wananchi.
“Ni vema mawaziri hawa wakafanya maombi kwa kuwaita au kuwafuata viongozi wa dini kwani wana kazi ngumu kulingana na nia njema aliyonayo Rais Magufuli katika kupambana na masuala ya ufisadi.
“… kazi ya kupambana na ufisadi kamwe si rahisi hadi kushangilia uteuzi, lengo kubwa ni kuwaletea wananchi maendeleo kupitia ubinafsishaji wa viwanda kutoka kwa watu waliomilikishwa na kuviua,” alisema Kinana.
Katibu mkuu huyo wa CCM, alisema anaunga mkono uamuzi wa Rais Magufuli wa kufuta maadhimisho ya Siku ya Ukimwi dunaini, hali ya kuwa wagonjwa hawana dawa.
“Nyingine ni Wiki ya Maji, mnafanya maadhimisho huku watu hawana maji, Wiki ya Maziwa wakati wafugaji wamekonda na mifugo imekonda haitoi maziwa, fedha hizo zitumike kwa mambo mengine,” alisema Kinana.
WABUNGE wanne wa CCM Wametajwa Kukataa Uteuzi wa Nafasi ya Uwaziri Wakihofia Kushindwa Kuendana na Kasi Magufuli
6
December 15, 2015
Haitujalishi siye achaguwe ridhiwani
ReplyDeleteTibaijuka
Na majizi yote ya CCM
Wala hatuna mshipa
Mchaguwe kinana aliyesema mawaziri WA kikwete mzigo umempa nape mpe naye jizi la Meno ya tembo na wanyama tena mpe maliasili na utaliiiiiiiii
ReplyDeleteNyinyi UKAWA kama huna maoni bora ukae kimya mie sisemi sana
ReplyDeleteHuyu Malaya bado yupo oops
ReplyDeleteMwanamke fukuza huyu
Janet huyu si msaidizi
Hata Obama hakaliwi hivi na walinzi wake kikwete umetuachia laana ya maisha
ReplyDeleteKwa urais gani Tanzania kiasi
Watanzania kwa vishindo
Magufuli Anzia na hawa walinzi au waandishi wasio kuwa na tija
Hivi kwanini Tanzania mtu lazima dr ........
ReplyDeleteMbona Obama na Ph.D. Lakini haitwi dr Obama
Kansela wa ujerumani ni dr tena kizikia
Haitwi dr agela
Tena wengine Ph.D. Feki na bado unawaita dr ..........
Siasa si taaluma jamani
Wanaiasa waitwe majina yao
Waandishi wa habari badilisheni hili