Wafanyakazi Wanne wa Serekali Wakiuka Amri ya Rais Magufuli ya Kusafiri Nje ya Nchi Bila Ruhusa ya Rais..Wafukuzwa Kazi

Rais Magufuli ameagiza kusimamishwa kazi mara moja kwa watumishi waandamizi wanne wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU ambao walisafiri nje ya nchi licha ya Rais Magufuli kupiga marufuku safari za nje kwa watumishi wa umma.

Watumishi hao ni Mary Mosha, Ekwabi Mujungu, Doreen Kapwani na Rukia Nikitas ambao walisafiri nje ya nchi licha ya kunyimwa kibali cha safari kutoka kwa Rais ama Katibu Mkuu Kiongozi.

Agizo hilo la Rais Magufuli  lilitolewa jana na Balozi Mkuu Kiongozi Ombeni Sefue wakati alipokuwa akiongea na waandishi wa habari.

Balozi Sefue amewataka watumishi wengine wa umma kutii agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na kuonya kuwa atakayekiuka atachukuliwa hatua kali.

Nafasi za Kazi

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. yaani ikipita siku sijaingia kwenye mitandao ya kijamii nahis kama ninaumwa. haya ndo mambo tuliyotaka na tunayopenda kuyaona kila siku kwenye vyombo vya habari. hadi inafurahisha jamani maana kusikia leo katolewa huyu mara kasimamishwa yule kwa uzembe wa wazi kabisa tena wa miaka nenda rudi kiukweli Rais wetu Magufuli ADUMU MILELE.

    ReplyDelete
  2. viva my presidaaaa viva

    ReplyDelete
  3. SAFI JPM KWA KUTUMBUA MAJIPU SUGU KWELI HAPAKAZITU

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad