Walichoongea Rais Magufuli Na Maalim Seif Baada ya Kukuta Ikulu Jijini Dar

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amekutana naMakamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Mgombea Urais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharrif Hamad, leo tarehe 21 Desemba, 2015 Ikulu Jijini Dar es Salaam  kufuatia maombi yake ya siku nyingi.

Mazungumzo ya Viongozi hao pia yamehudhuriwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Viongozi hawa kwa pamoja wamejadili hali ya kisiasa Zanzibar na wamefurahishwa na hali ya usalama na utulivu inayoendelea.

Aidha, Mhe. Rais Magufuli amewapongeza Rais wa Zanzibar Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein, Makamu wa Kwanza wa Rais  wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, na viongozi wote wanaoshiriki katika mazungumzo ya kuleta hali ya uelewano Zanzibar.

Rais Magufuli pia  amewapongeza na kuwashukuru wananchi wa Zanzibar kwa kudumisha amani na utulivu wakati wa mazungumzo baina ya viongozi wa CUF na CCM yakiendelea huko Zanzibar.

Katika Mazungumzo hayo Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar Maalim Seif Sharrif  Hamad amemueleza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania juu ya hali ya siasa Zanzibar kadiri anavyoielewa yeye na Rais Magufuli amemshukuru Makamu huyo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar kwa taarifa yake nzuri huku akimsihi waendelee na mazungumzo hadi suluhisho muafaka lipatikane.

Majadiliano yanayoendelea yanatoa fursa ya kudumishwa kwa utulivu na sifa njema ya nchi yetu. Wote kwa pamoja wamewaomba wananchi waendelee kuwa watulivu ili kutoa nafasi ya majadiliano yanayoendelea kufikia hatma njema.

Wameelezea matumaini yao kuwa vyama vya CCM na CUF haviwezi kushindwa kupata suluhu ya mgogoro huo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amemuhakikishia kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano itahakikisha kuwa amani na utulivu unaendelea kudumishwa Zanzibar.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU.
21Desemba, 2015

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. SULUHU KUBWA NI KUMTANGAZA ALIYESHINDA NGOJA NGOJA INAUMIZA MATUMBO

    ReplyDelete
    Replies
    1. Siku zote ukweli unauma na haupatikani.Demokrasia ipo baadhi ya nchi.wanaangalia Maslahi yao sio Demokrasia.
      HAMAS ilishinda Palestine lakini PLO ndio yenye Maslahi

      Delete
  2. SIJAMSIKIA RAIS MHESHIMIWA MAGUFULI AKITOA MWITO KWAMBA MAAMUZI YA WAZANZIBARI WALIO WENGI KAMA YALIVYOJIONYESHA WAZI SIKU YA UCHAGUZI MKUU JUMAPILI TAREHE 25,OCTOBA 2015 YAHESHIMIWE NA,MSHINDI APEWE USHINDI,HAJATAMKA NA HAKUKUSUDIA KUTAMKA HIVYO. UNAJUA KWA NINI? KWA SABABU USHINDI WA ZANZIBAR UPO KWENYE ILAANI YA CCM.MHESHIMIWA RAIS HAWEZI KWENDA KINYUME NA MAAMUZI NA UTASHI WA CCM KUHUSU UTAWALA WA ZANZIBAR.CCM ITAGAWANYIKA,ITAPUKUTIKA. .CCM NDIYO ILIYOMUWEKA HAPO,NI LAZIMA AILINDE. NINACHOKIONA NI MAJARIBIO YA CCM KUENDELEA NA VUNGA LA NGUVU,KUPOTEZA MUDA. LEO HII TUMJADIRI NA ITUPELEKEE KUMHUKUMU JAKAYA MRISHO KIKWETE YEYE NDIYE ALIYESABABISHA SINTOFAHAMU HII WAKATI HUO AKIWA NDIYE MKUU WA NCHI. NAONA MAZUNGUMZO YEYOTE KUWA YASIYOFAA WALA KUWA NA MAANA KWA WANANCHI, KWANI TUNAZIDI KUGADHABISHWA.NI NDOTO ZA MCHANA KWA CCM KUKUBALI UKWELI,TENA UKWELI WA MUNGU,KWAMBA MSHINDI WA KURA ZA URAIS ZANZIBAR NI SEIF SHARIFF HAMAD WA UKAWA-CUF-ZANZIBAR. MIMI NAONA,KWAMBA,MAGUFULI NI MWANACHAMA WA KAWAIDA WA CCM NA MWENYEKITI WAKE NI JAKAYA MRISHO KIKWETE.NAONA HILI LA ZANZIBAR TUACHIWE WAZANZIBARI WENYEWE.RUKSA ZA MIKUTANO SASA ZIFUNGULIWE, KWANI HIVI SASA UDIKTETA,VITISHO,UKANDAMIZAJI ZANZIBAR UNAZIDI KUSHIKA KASI.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad