Wastara: Najuta Starehe Zimeniponza

STAA wa filamu Bongo, Wastara Juma amesema kitu ambacho kimemponza na kumfanya asumbuliwe na mguu wake mara kwa mara ni kujisahau sana katika starehe kwa kuwa hajawahi kujikubali kuwa ni mlemavu.

Akipiga stori na paparazi wetu Wastara alisema, tangu alipopatwa na tatizo hilo la mguu kwenye fikra zake hakutaka kukubali matokeo, siku zote alipenda aishi kama alivyokuwa mzima ikiwa ni pamoja na kwenda kwenye muziki na kucheza.
“Siyo siri nilijisahau sana, sikupenda kujiona mlemavu, nilikuwa naishi kama mtu wa kawaida tu.
Sasa hivi najuta kwa kutozingatia matunzo ya mguu wangu maana nilikuwa najiachia sana hususan linapokuja suala la muziki. Sasa nimeamua kukubaliana na hali halisi kama walivyo walemavu wengine,” alisema Wastara.

Chanzo:Global Publishers
Tags

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Pole basi Tulia usijitoe sana mitandaoni
    Binadamu wote si wema kwani unahitaji msaada WA kiti

    ReplyDelete
  2. najua upo katika wakati mgumu sana kwa kupoteza kiungo kimojawapo mwilini ni inahitaji moyo kukubali na akili huwa inaathirika kiaina. cha msingi kwa sasa acha maisha ya anasa mtafute Mungu. pole sana mpendwa.

    ReplyDelete
  3. tulia sasa achana na skendo za kiboya

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad