Waziri Mkuu Ataka Amani ya Nchi Ilindwe......Akemea Uvaaji wa Nguo Fupi na Matumizi Ya Dawa Za Kulevya

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amewataka wananchi waendelee kulinda amani ya nchi huku akikemea uvaaji wa nguo fupi na kuwasihi Watanzania kujenga tabia ya kuvaa mavazi yenye kumpendeza Mungu.

Pia, amekemea matumizi ya dawa za kulevya na mimba za utotoni akisema ni mambo ambayo yanaepukika kwa mtu yeyote aliyelelewa katika misingi ya kidini.

Waziri Majaliwa alisema hayo jana alipokuwa akihutubia Baraza la Maulid lililofanyika Karimjee jijini Dar es Salaam.

Alisema mambo yote hayo yanawezekana kama watu watamkimbilia Mungu huku akiwaomba viongozi wa dini kuwausia waumini wao kuvaa mavazi ambayo yanampendeza Mungu.

“Mtoto akilelewa kwenye mazingira ya dini itakuwa ngumu kuvaa mavazi ambayo hayampendezi Mungu,” alisema.

Amesema Serikali itaendelea kushirikiana na taasisi za kidini zile ambazo ziko kisheria huku akizitaka ziendelee kuisaidia Serikali kwa kujenga shule na hospitali na kutoa huduma nyingine za kijamii.

Waziri Majaliwa alitumia fursa hiyo kuwapongeza Watanzania kwa kuwa watulivu katika kipindi chote cha uchaguzi hadi ulipofanyika Oktoba 25.

Akizungumza katika baraza hilo, Sheikh Mkuu wa Tanzania, Mufti, Abubakari Zuberi aliwaasa waumini wa Kiislamu kufanya mambo yote yanayompendeza Mwenyezi Mungu.

Aliwashukuru Waislamu wote nchini kwa kushirikiana na wananchi wenzao ambao siyo wa dini hiyo katika kudumisha amani.

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kaanza upuuzi huyu nae. Nguo fupi sio jambo la kuzungumzia, kuna mambo kibao ya maana yanayohusu maendeleo ya nchi. Vipi majipu, naona mnayakaushia sasa na mnabadili upepo.

    ReplyDelete
  2. Wewe anony wa saa 1:37pm ndiyo mpuuzi. Mavazi yasiyo ya staha ni jambo baya. Nchi za Kiarabu ndizo zenye kiwango cha chini cha maambukizi ya VVU. Afrika Kusini wanaojifanya wajuaji wa kuvaa vibaya ni miongoni mwa nchi zenye kiwango kikubwa cha maambukizi ya VVU na vitendo vya ubakaji. Wewe endelea kudhani si wakati wake kuzungumzia hili janga.

    ReplyDelete
  3. Naye aache kutia mywele rangi nyeusi kichwani

    ReplyDelete
  4. hata uvaaji wa nguo fupi ni ufisadi na uvunjaji wa maadii na kama kiongozi na mzazi na mtanzania mwadilifu ni haki yake kukemea na watu wote tumuunge mkono
    we ujipitishe na kinguo chako kifupi ukichaniniwa unalalamika afterow unawaweka watu ktk majaribu
    maadili yanavunjika na ndo apo ile me bepari ya ulaya inatumia mwanya huo kutuletea ndoa za jinsia moja na mauchafu kibao
    majaliwa safi sana na kwanza wewe ni waziri mkuu wa kwanza kutoa kauli ya namna hii lazima heshima iwepo
    wataelewa tuu mema yako muheshimiwa

    ReplyDelete
  5. Hakuna lolote! Tabia na mavazi ni vitu viwili tofauti. Kuna wanaojifunika kucha mpaka nywele, na ni malaya kupindukia. Wewe unayechana wenye nguo fupi hali huwajui, inaonyesha jinsi ulivyo na malezi mabovu. Msihukumu kitabu kwa rangi yake!!!!.

    ReplyDelete
  6. Muulizeni Shamsa Ford KUHUSU MAVAZI MAFUPI

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad