Waziri Mpya wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Makame Mbarawa Avamia DAWASCO Kwa Kushtukiza..Atoa Maagizo Haya

Profesa Makame Mbarawa 
Waziri mpya wa maji na umwagiliaji, Profesa Makame Mbarawa, ameiagiza mamlaka ya maji safi na maji taka jijini Dar es Salaam DAWASCO, kuongeza idadi ya watu wanaotumia maji safi kutoka 148,000 (idadi ya sasa) hadi watu 1,000,000 kufikia Juni mwaka ujao.

Profesa Mbarawa alitoa agizo hilo alipofanya ziara ya kushtukiza katika makao makuu ya DAWASCO. Mbarawa amesema serikali ya awamu ya tano imejizatiti kuhakikisha kunakuwa na maji salama na wanawake hawapati shida ya kutembea umbali mrefu kutafuta maji.

Kati ya mambo aliyoahidi Rais Magufuli wakati wa kampeni zake, ni kuweka mikakati ya kuhakikisha kunakuwepo na maji safi na salama ili kumaliza tatizo la ukosefu wake lililopo tangu nchi ipate uhuru.

Rais Magufuli pia alisisitiza kuwa Serikali yake haitavumilia mawaziri wavivu, hasa waliopewa wizara nyeti kama hii ya maji.

Mbawara pia ameagiza kuwepo na bei nafuu ili kila mwananchi aweze kupata maji safi na salama.

Tarehe 1, mwezi huu wa 12, DAWASCO ilipandisha bei ya maji kutoka shilingi 1, 098 kwa lita 1000 hadi shilingi 1,663 kwa kipimo hicho.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad