Waziri Nape Akanusha Wizara Yake Kukataza Wanawake Kuvaa Mavazi ya Kubana

Waziri wa Habari, Utamaduni Wasanii na Michezo Nape Nnauye, amekanusha taarifa iliyosambaa mitandaoni inayohusu wizara yake kukataza baadhi ya mavazi hasa sehemu za mikusanyiko ya umma.

Amesema Taarifa hizo ni za uzushi na uongo, na kuwataka mamlaka husika kuwachukulia hatua watu waliotoa taarifa za uongo.

Hizo taarifa ni uzushi mtupu na uongo, mamlaka husika wachukue hatua, watimize wajibu wao, watumie sheria iliyopo kuwachukulia hatua”, amesema Mh. Nape Nnauye.

Mwishoni mwa wiki hii kuna taarifa ilisambaa kwenye mitandao ya kijamii ikionyesha ni taarifa kwa vyombo habari juu ya katazo la mavazi yasiyofaa kwenye mikusanyiko ya watu, hususan hospitali, maofisini, sokoni, na vyuoni.

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mie ningeshukuru mungu na ningefurahi ingekuwa haya maneno kweli..sababu hasara tunazopata na mavazi haya ni makubwa maana vizazi vinapotea ,ukimwi unazidi maana haya mavazi yanashawishi sanaa na ni chanzo la.ongezeko la ukimwi..mtu unavaliwa nusu uchu mchani upo na familia yako aibuuuu sisi tulikuwa sio hivi tufate mila zetu jamani sisi tulikuwa tunajivunia kwa stara lkn sahivi hurumaaa kabisa.sasa watoto hawasomi wanafata starehe mzazi ana dhibiti mpaka anachoka vishawishi wingi...na ndo maana tukaambiwa wanawake wengi wataingia motoni ndo tunashawishi watu wafanye madhambi jamaniii

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad