Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee Ummy Mwalimu amefanya ziara ya kushtukiza katika Hospitali ya Taifa Muhimbili leo na kukuta mashine za CT Scan na MRI hazifanyi kazi.
Katika ziara hiyo aliyoifanya asubuhi ya leo, alikutana na mzee wa miaka 90 ambaye alikuwa akisubiri huduma hiyo tangu jana.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi Wa Hospitali hiyo, Lawrence Museru, mashine hizo ziliharibika tangu juzi na hivyo huduma zilisimama tangu jana asubuhi.
Tatizo kubwa katika machine ya CT Scan picha hazisomeki vizuri na MRI imeharibika spea ambazo kwa mujibu wa uongozi wa hospitali hiyo, matengenezo yanaanza leo.
Hata hivyo, Mwalimu ameagiza uongozi wa hospitali hiyo ya rufaa kuchukua hatua madhubuti kuhakikisha kuwa mashine hizi zinarudi katika hali yake ya kawaida.
Mashine hizo zimeendelea kuwa changamoto kwa hospitali hiyo licha ya Rais John Magufuli kufanya ziara ya kushtukiza na kukuta hali kama ya leo.
Huu sasa umekuwa upuuzi!! Inaonekana mashine zilinunuliwa kinyemela na wapigaji, hata guarantee hazina!! Yale yale, wale wale, ile ile.
ReplyDeleteKilasiku zikitengenezwa Wanaziaribu kwa makusudi ili hospitali zao binafsi waingize ela
ReplyDeleteMkapa alisema 2010
ReplyDeleteMsichaguwe rais kwa uzuri wa sura
Na tumeoona 10 years
Madeni , ufisadi, meno ya tembo
Masikini wanaofukuzwa kazi Leo Hawana makosa makosa ni yule aliyekuwa akiwakingia kifua Na kula nao
Ikulu ilkuwa si ikulu
Magufuli rudisha hadhi ya ikulu