Waziri wa fedha Dr. Philip Mpango, akataa kuwa Waziri ombaomba

WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango amesema kamwe hatapenda kuwa waziri ombaomba wa fedha, bali atahakikisha anaelekeza nguvu katika kukusanya kodi ili nchi iweze kujitosheleza kwa mapato ya ndani.

Aidha, amesema atahakikisha mifumo ya kodi inakuwa rafiki kwa wafanyabiashara na wawekezaji ili wasikimbie kulipa kodi, huku akiahidi kuangalia jinsi ya kuachana na kodi zenye kero kwa Watanzania.

Aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam wakati alikabidhi ofisi kwa Kaimu Kamishna Mkuu mpya wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Alphayo Kidata.

Kabla ya kuteuliwa kuwa Waziri wa Fedha wiki iliyopita, Dk Mpango alikuwa Kaimu Kamishna Mkuu wa TRA, wakati Kidata alikuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

“Sipendi kuwa waziri wa kuombaomba hivyo nitaelekeza nguvu zangu katika ukusanyaji kodi na kuona nchi yetu inajitegemea kwa mapato ya ndani kwa kiasi kikubwa, lakini ili kufanya hivyo ni lazima kuziba mianya ya mapato…” alisema Dk Mpango.

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. SAWASAWA DOKTA,LAKINI UWE MWANGAIFU SANA KWA SABABU SASA HIVI MTANZANIA WA KAWAIDA TAYARI AMEKWISHAELEMEWA NA MZIGO MKUBWA WA UTITIRI WA KODI.KUKAMULIWA ZAIDI LITAKUA TATIZO ZITO NA UTAUA ARI YA KUFANYA KAZI KWA NGUVU NA HIVYO KUDUMAZA UCHUMI NA MAENDELEO.UWE MWANGALIFU SANA,NA TUTALIONA HILO KWENYE BAJETI YAKO YA KWANZA MWAKANI.KIMATAIFA TANZANIA INA MADENI YA MATRILLION YA SHILINGI NA TUNADAIWA NA TAASISI MBALI-MBALI ZA WAKOPESHAJI WA KIMATAIFA.JEE UTAYAHESHIMU MADENI YALE KAMA YAIVYO AU UTAIPITIA UPYA MIKATABA YA UKOPAJI YA NYUMA MINGI IKIWA IIYOGUBIKWA NA USANII KIBAO,WIZI KIBAO NA MPAKA SASA UKIMYA KIBAO.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad