Wema Sepetu Kortini Kwa Uwizi wa Umeme..Tanesco Waeleza Makubwa

KIMENUKA! Baada ya Miss Tanzania 2006 aliye pia nyota wa sinema za Bongo, Wema Sepetu ‘Madam’ kunaswa na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) akidaiwa kutumia umeme wa shirika hilo kinyemela, kuna madai atapandishwa kortini.
Taarifa kutoka chanzo makini zinasema kuwa, mrembo huyo alifanya ‘manuva’ hayo katika nyumba anayoishi, Kijitonyama, Dar hivyo kuweza kuliingizia hasara shirika hilo hali ambayo shirika hilo haliwezi kumvumilia.


“Amefanya ile michezo ya kuchezea mita. Mita inakuwa inasoma umeme mdogo lakini mzigo unaotumika ndani mkubwa, haufanani na malipo halisi ambayo alistahili kulipia,” kilisema chanzo chetu na kuongeza:
“Maofisa wa Tanesco juzikati ndiyo wakampitia. Inasemekana Wema alikuwa ndani na Idris (yule mshindi wa Big Brother Africa). Idris ndiye alitoka lakini Madam hakuinua miguu yake kwenda nje, wakamng’olea mita na kuondoka nayo.”

Baada ya chanzo hicho kuvujisha ubuyu huo sambamba na picha zilizosemekana ni za siku ya tukio wakati maofisa hao walipofika nyumbani hapo na kufanya ‘ambushi’, paparazi wetu alimpigia simu Wema kwa muda mrefu lakini hakupatikana, akampigia mtu wa karibu na Madam, Ahmed Hasheem ‘Petit Man’ ambapo alipatikana na kusema:

“Unajua kaka mimi si msemaji wa Wema. Mimi ni msemaji wa wasanii walio kwenye lebo ya Wema ya Endless Fame. Kama unataka msemaji wake, cheki na Martin Kadinda.”
Alipotafutwa Martin, alijibu kwa kifupi: “Kaka hata mimi nazisikia hizo habari lakini sipo Dar, nikirudi nitakwenda kucheki halafu nitakupa taarifa kamili.”
Juzi Jumanne, paparazi wetu alifika nyumbani kwa Wema ili kujionea sakata hilo lakini hakufanikiwa kuingia getini baada ya kugonga geti kwa muda mrefu bila majibu.
Mmoja wa majirani wa mrembo huyo aliyeomba hifadhi ya jina, alipoulizwa kuhusu kufahamu sakata hilo, alisema:

“Kiukweli sisi wenyewe tulishangaa. Tunaamini Madam si mtu kuchezea mita. Ni mtu anayejiweza, anayejitambua sasa tumeshtuka kuona mita inatolewa.”
Paparazi wetu alifika Ofisi za Tanesco Mkoa wa Kinondoni Kaskazini (Mikocheni) ili kuzungumza na wahusika lakini akakosa ushirikiano.

Hata hivyo, mfanyakazi mmoja wa Kitengo cha Emergency (Dharura) aliyeomba kufichwa jina lake, alisema ni kweli zoezi hilo lilifanyika nyumbani kwa Wema, Jumatatu iliyopita na kukutana na kadhia hiyo ambapo alisema madam huyo atapandishwa mahakamani kujibu mashitaka ya kuiibia Tanesco.
GPL

Post a Comment

12 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mama ongea na mwanao

    ReplyDelete
  2. haya karibuni watoa komenti za chuki hapa mjimwage

    ReplyDelete
    Replies
    1. SAWA SAWA NDUGU.WATAJWE WOTE WANAOSHIKWA .MUSIPOSHANGAA ZAIDI.

      Delete
  3. Msilikuze sana
    Kwani wezi umeme wapo wengi sana bongo
    Tulaani mfomo uliopita watu walikuwa wathamini kazi
    Inawezekana kabisa hao hao tanesco hufuata wateja na kufanya deal nao

    ReplyDelete
  4. Hapa kazi tu,tunaongea ukweli hamna comment za chuki wala nini kama hupendi ukweli meza sumu ya panya.

    ReplyDelete
  5. ukweli gani uloongea zaidi ya kufata kiki, TRA wameiba mabillio hamkuona itakuwa umeme wa elfu 50. kajambe mbele Anony 4.30 PM

    ReplyDelete
  6. Mamam sema na mwanao hapa kazi tu!=kasi zaidi nguvu zaidi!= kasi mpya ari zaidi! = kucheza na mind za waliolala= nchi inayoendeshwa kwa ziara za kushitukiza haina mifumo imara ya kuliendesha taifa= ukweli!

    usipojiamsha mwenyewe hakuna wa kukuamsha!

    ReplyDelete
  7. Kutokulipa deni kisheria ni kosa iwe tsh100 au maelfu mamilioni mabilioni matrilion hajalishi kitu inabaki kuwa vile vile ni kosa either ulipe au ufikishwe mbele ya pilato ukajibu mashtaka hakuna haja ya kumtetea mtu kama dizaini hiyo hata awe nani kosa ni kosa tu fullstop

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ni kweli kosa ni kosa .je wangapi wanafanya hayo makosa? mbona majipu hayo hayatumbuliwi?

      Delete
  8. balaa, ningekuwa wema nikiitwa mahakamani nawageukia wao wenyewe, make ni kazi yao kutambua umeme unaotumika na mfumo wa umeme katika nyumba ya wema, unaendana na matumizi yenyewe? NAWAAMBIA MIE SIJASOMEA UMEME, MIE MSANII, WENYEWE NDIYO WANAHUSIKA, KAMA MITA ILIKUWA MBOVU MIE NINGETAMBUA VIPI? KILA MWEZI WANASOMA MITA MBONA HAWAJAWI SEMA, WENYEWE NDIYO WALIFUNGA MIE SIJUI.

    ReplyDelete
  9. Alaumiwe kikwete aliyembebabeba

    ReplyDelete
  10. Alaumiwe kikwete aliyembebabeba

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad