Zanzibar: Dr. Shein yuko Tayari kwa Lolote; Maalim Seif Anataka Moja tu

Alipokuwa akizungumzia kufutwa kwa uchaguzi mzima wa Zanzibar, aliyekuwa mgombea wa CUF, Maalim Seif Sharrif Hamad alisema safari hii 'No compromise'. Ingawa ni sentensi fupi, ina ujumbe mzito. Ujumbe wa Maalim Seif ni kuwa safari hii hatakubali kuombwa na hatimaye kukubali matokeo kama ilivyokuwa miaka ya 2005 na 2010. Kauli ya kuwepo kwa 'compromise' inathibitisha kauli ya Mzee Moyo aliyosema kuwa ilifika wakati aliombwa akamshawishi Maalim Seif akubali matokeo.

Maalim Seif ametuma ujumbe mmoja mkubwa. Ujumbe wa kutotakiwa tena mashauriano ya kumfanya abadili msimamo wake wa kutangazwa mshindoi wa uchaguzi wa mwaka huu ambao umefutwa na Mwenyrkiti wa ZEC, Ndugu Jecha. Maalim Seif, pamoja na kufanya mazungumzo ya hapa na pale; ya huyu na yule, anataka jambo moja tu: mshindi atangazwe na mambo mengine yaendelee.

Wakati Maalim Seif akisema na kubaki na msimamo huo, Dr. Ali Mohamed Shein, Rais wa Zanzibar na aliyekuwa mgombea wa CCM, yuko tayari kwa jambo lolote. Yuko tayari kutangazwa kwa mshindi; yuko tayari kurudiwa kwa uchaguzi na kadhalika. Msimamo huo unachagizwa na heshima ya Dr. Shein katika kufuata na kutii makubaliano ya Muafaka uliopelekea kuundwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa.

Pia, 'upemba' wa Dr. Shein na Maalim Seif unakoleza msimamo wa lolote-lije wa Dr. Shein. Dr. Shein anamuona Maalim kama ndugu na Mwalimu wake wa kisiasa na hata kaka wa kisiasa. Lakini, external forces from party members and party leaders make things harder for Dr. Shein. He is afraid of being named a party traitor!

Source: Jamii Forums/Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad