Zitto Kabwe Achekelea Utabiri Wake Kutimia Zanzibar....Majeshi Yaanza Kuondolewa

KIONGOZI wa chama cha ACT-Wazalendo Zitto Kabwe ameelezwa kufurahishwa na jitihada za kumaliza mzozo wa kisiasa visiwani Zanzibar,huku akitaja baadhi ya mbinu ambazo chama chake waliishauri Serikali ambazo zimeanza kuchukuliwa hatua.

Hii hapa chini ni post yake katika mtandao wa facebook juu ya suala hilo

Zanzibar tartiibu….

Disemba 20 mwaka huu 2015 Kamati ya Uongozi ya Chama cha ACT Wazalendo ilitoa tamko lake baada ya kufuatilia hali ya Zanzibar.

Moja ya mambo yaliyoelezwa katika tamko hilo ni uwepo wa askari wengi katika kisiwa hicho hali iliyokuwa inatishia amani kwa wananchi

Taarifa hiyo ya ACT mbali na masuala mengine, ikaeleza kuwa ni wakati muafaka kwa serikali kuhakikisha inawarudisha askari hao wa vikosi mbali mbali kuanzia jeshi la Polisi,JKU,KMKM JWTZ na Mafunzo katika makambi yao.

Lengo likiwa ni kuwaacha wananchi wakiwa katika uhuru wa kufanya shughuli zao wakati suala la mtanziko wa kisiasa kisiwani humo ukiwa unafanyiwa kazi

Kuanzia jana Disemba 22 na leo Disemba 23 majeshi hayo yameshaanza kuondoka katika maeneo mbali mbali ya mji wa Znz hali inayoashiria mwanzo wa mwisho mwema katika kadhia ya uchaguzi wa Zanzibar.

Ninaomba mamlaka husika ziendelee kufanyia kazi mapendekezo yetu mengine ili kulimaliza kabisa suala hili.

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Huyu naye sijui huko kigoma anafanya kazi saa ngapi? Yeye na serikali tu muda wote hebu rudi kigoma kwanza mji huu maendeleo yako nyuma mno kiherehere hicho kilete huku sisi ndo tuliokupa kura tufanyie kazi

    ReplyDelete
  2. Kuchu huyu
    Kama nape na Makonda
    Kikwete katuachia vidonda
    Fyuuuuuuuuuuuuuu

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mwacheni atimize wajibu wake,ni kitanzania kiongozi wa kitaifa sio wa kikanda wala jimbo pekee,anathamini wote,Zanzibar na Tanganyika.

      Delete
  3. Mwanasiasa wa kizazi cha Leo mwenye maono ya kitanzania kwa ujumla na si ukabila na ukanda,mwacheni atimize majukumu yake kitaifa.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad