Zitto Kabwe Afunguka Mazito..Awataka Baadhi ya Wanasiasa Kuacha Siasa za Porojo

Mbunge wa Kigoma mjini kupitia chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe amefunguka na kuwataka baddhi ya wanasiasa kuacha siasa za porojo na kuangalia masuala ya msingi na sio uteuzi wa Prof. Sospeter Muhongo.

Zitto Kabwe ameyasema haya kupitia mtandao wake wa kijamii wa facebook siku kadhaa baada ya Mbunge wa Kibamba kupitia tiketi ya Chadema . John Mnyika kudai kuwa atafufua sakata la Escrow bungeni kufuatia uamuzi wa Rais John Pombe Magufuli kumteua Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo.

"Prof. Sospeter Muhongo alikuwa Waziri wa Nishati na Madini wakati wa sakata la ‪#‎TegetaEscrow‬. Kamati ya Bunge ilipendekeza na Bunge kuazimia kuwa Muhongo avuliwe madaraka yake ya Uwaziri. Prof. Muhongo alijiuzulu. Akafanyiwa uchunguzi na Kamishna wa Maadili kutamka kuwa hakukutwa na kosa la kimaadili" Alisema Zitto Kabwe

Lakini Mbunge huyo alizidi kusikitiza kuwa "Unajengaje hoja kuwa hana haki ya kuteuliwa kuwa Waziri? Keshaadhibiwa kwa kosa la awali, kwa kujiuzulu. Sheria ipi inasema hana haki ya kuteuliwa tena? Niliongoza Kamati ya PAC. Nina uhakika Waziri muhongo kwenye sakata lile alishauriwa vibaya na kujikuta anatetea ubadhirifu. Lile nifunzo kubwa kwake na ninavyomuona sasa hatarudia tena makosa yale. Kuna mambo ya msingi lazima afanye sasa

1) Azuie kuanzia sasa malipo ya 'capacity charges' kwa kampuni ya kitapeli ya IPTL na atumie sheria kutwaa mitambo ya IPTL na kumilikisha TANESCO
2) Amtake Waziri wa Mambo ya Ndani na Jeshi la Polisi kumkamata mara moja anayejiita mmiliki wa IPTL na afunguliwe mashtaka ya utapeli, wizi wa udanganyifu na uhujumu uchumi; huyo mmiliki na washirika wake ambao ni raia wa Tanzania

3) Amtake Gavana wa Benki Kuu na FIU kuichukulia hatua za kisheria Benki ya Stanbic ikiwemo kupiga faini ya kurejesha fedha zote zilizokua kwenye akaunti ya Tegeta Escrow.
Hizo ndio hoja za msingi na sio uteuzi wa Prof. Muhongo. Mwenye ushahidi dhidi ya Muhongo si aende Mahakamani? Tuache siasa za porojo porojo" Alisisitiza Zitto Kabwe.

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kula 5 Muheshimiwa Zitto. Unafikiri watafanyaje kwa sasa zaidi ya 'porojo-porojo', hawana jipya, kifupi WAMEISHIWA HOJA ZA MSINGI, wamebakiza 3 tu MIKUTANO YA HADHARA, MAANDAMANO NA PRESS CONFERENCE

    ReplyDelete
  2. Tibaijuka naye arudishwe

    ReplyDelete
  3. Zitto kabwe karibu ccm tunajua wewe ni wetu tumekutumia chadema,please come back home.

    ReplyDelete
  4. Wamemshindwa wale walikabidhiwa kumlea na kumwangalia itakuwa nyinyi CCM
    Na jeuri ya ushawishi Na ubishoo
    Ni kijana mzuri sana mjenga hoja lakini huwa anafikiri anajuwa kuliko wengine

    ReplyDelete
  5. We Zitto jeuri, pia mwanasiasa. Kujiuzuru si adhabu. Mtu akijiuzuru lazima alipe makosa aliyoyafanya. Usitinge Watanzania ukajiona ni wewe pekee unaakili. Mbona wengine mmewafunga, mmewapeleka mahakamani. Hii chagua italeta usawa gani. Hii ni sheria gani. Watu tunajua sheria si wewe peke yako. Ulikuja juu Escrow leo unamtetea. Werwe acha siasa za CCM na ufuate haki na kupigania maslahi ya Watanzania. Wewe uwe sauti ya watu badala ya kuwa kinyonga. Acha upuuzi na kuwachanganya Watanzania. Acha kupigania maslahi binafsi,. Najua unataka kuwa raisi, bahati mbaya huna msimamo kamili. Unataka upendwe upande kazi. Najua ni msomi, hujawa msoimi pekee. Wabane Akina Kikwete unaocheka nao. Hapa nitakusifu.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad