Waliosema Ufisadi ni Mfumo ndio wanasema leo Prof. Muhongo hafai kuwa Waziri sababu ya Tegeta Escrow. Sijui lini mahakama ilimhukumu Muhongo! Sijui lini Muhongo kawa Mfumo. Tujifunze kuweka akiba.
Prof. Sospeter Muhongo alikuwa Waziri wa Nishati na Madini wakati wa sakata la TegetaEscrow.
Kamati ya Bunge ilipendekeza na Bunge kuazimia kuwa Muhongo avuliwe madaraka yake ya Uwaziri. Prof. Muhongo alijiuzulu.
Akafanyiwa uchunguzi na Kamishna wa Maadili kutamka kuwa hakukutwa na kosa la kimaadili. Unajengaje hoja kuwa hana haki ya kuteuliwa kuwa Waziri?
Keshaadhibiwa kwa kosa la awali, kwa kujiuzulu. Sheria ipi inasema hana haki ya kuteuliwa tena?
Niliongoza Kamati ya PAC. Nina uhakika Waziri muhongo kwenye sakata lile alishauriwa vibaya na kujikuta anatetea ubadhirifu.
Lile nifunzo kubwa kwake na ninavyomuona sasa hatarudia tena makosa yale. Kuna mambo ya msingi lazima afanye sasa
1) Azuie kuanzia sasa malipo ya 'capacity charges' kwa kampuni ya kitapeli ya IPTL na atumie sheria kutwaa mitambo ya IPTL na kumilikisha TANESCO
2) Amtake Waziri wa Mambo ya Ndani na Jeshi la Polisi kumkamata mara moja anayejiita mmiliki wa IPTL na afunguliwe mashtaka ya utapeli, wizi wa udanganyifu na uhujumu uchumi; huyo mmiliki na washirika wake ambao ni raia wa Tanzania
3) Amtake Gavana wa Benki Kuu na FIU kuichukulia hatua za kisheria Benki ya Stanbic ikiwemo kupiga faini ya kurejesha fedha zote zilizokua kwenye akaunti ya Tegeta Escrow.
Hizo ndio hoja za msingi na sio uteuzi wa Prof. Muhongo. Mwenye ushahidi dhidi ya Muhongo si aende Mahakamani? Tuache siasa za porojo porojo
By: Zitto Kabwe
Zitto Kabwe Amtetea Prof Mohongo Kwa Kuchaguliwa Kuwa Waziri, Adai Mwenye Ushahidi Dhidi ya Muhongo Aende Mahakamani
12
December 17, 2015
Tags
Dooh!! Kama mambo ndio haya, hashitakiwi mtu,maana Eddo msafi, Lodi Lofa msafi,Tezi Dume msafi,Mama wa hela za mboga msafi, mradi hakuna wa kumpeleka mtu mahakamani, Mdau wa NEC aendelee na vichunusi tu,maana hatogusa jipu hata moja!!
ReplyDeleteHuyu kinyonga zito shughulikia matatizo ya jimbo lako acha kuwa mshabiki wa damu,na mimi nakushauri urudi ccm.
ReplyDeleteZitto kaka karibu ccm
ReplyDeleteachana na wanaume wavaa madela, kelele nyingi hawana lolote. kama vp waende mahakaman
ReplyDeletezito anatafuta ulaji ccm huyu, hamna lolote
ReplyDeleteNini tofauti ya lowassa na muhongo katika kashfa zinazowahusu. Ili zito aonekane mwongo. Tuache siasa. Tatizo cdm umeharibu wenyewe ajenda za kitaifa za kupambana na mafisadi. Zito yuko safi hata Kama mtamtukanaje he is always stable. Safi sana zito na Watajua umuhimu wako na Dr slaa ktk kuijenga cdm.
ReplyDeletesiku zote ukisema ukweli lazima upate maadui. Zito wewe ni mkomavu kisiasa na hakika utafika mbali kwa kusema ukweli achana na siasa za akina fulani kutafuta headline kila siku cha maana wanachokifanya hakuna
ReplyDeleteZITTO ACHA KIGEUGEU WEWE NDIO ULISEMA BUNGENI KUWA MUHONGO KAPEWA MGAO ESCROW
ReplyDeletehivi kamati ya ESROW alikuwa inaongozwa na nani?
ReplyDeleteZito si ulikuwa kamati ya escrow na wewe ulisema muhongo anahusika moja kwa moja sasa inakuaje leo watu wasihoji?mwisho wako wa kisiasa umefika na utaishia bungeni.
ReplyDeleteMsishangae jamani mtoto mdogo tizamani sura yake ana miaka 120
ReplyDeleteKazeeka umri na akili
Chadema walimjua wakamfukuza
Yupo CCM huyu
mmh.unatumia maneno makali mno...
ReplyDelete