Ali Kiba Anaamini Kutoa Nyimbo Nyingi ni Kutojiamini


Ali Kiba
Hitmaker wa Mwana,Ali Kiba amedai yeye anamini kutoa nyimbo Mara kwa Mara ni kutojiamini na ufujaji wa kipaji.

Mwimbaji huyo ambaye amekuwa akishinikizwa na mashabiki wake kuachia wimbo mpya ikiwa ni miezi kadhaa toka aachie video ya wimbo wa 'Cheketua',alikimbia kipindi cha The Sporah Show cha Clouds TV kuwa yeye akitoa kazi yake moja ina uwezo wa kukaa sokoni kwa muda mrefu.

"Fans don't worry about me,kitu ambacho nafanya "New Kiba,New Year" ni kutaka kwenda sawa na nyie.Lakini nilikuwa nataka mnielewe kutoa nyimbo kila dakika ni umalizaji wa Talent yako au kutojiamini auTalent yako fupi au una jaribu.Mimi najiamini kwa kitu ambacho natoa ni muda gani natakiwa kurudi tena",alisema.

Aidha,Ali Kiba aliwataka watu kuacha kumfananisha na wasanii wengine kwa kuwa yeye anafanya vitu tofauti na wengine.

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Enter your comment...Yeah, ni kweli kabisa kutoa nyimbo mara kwa mara umpoteza msanii km kweli anakitumia kipaji, Style yakutoa nyimboa kila wakati ni nidhamu ya uwoga na kutojiamin na wengi wenye style hiyo uwa wasipotoa nyimbo mfululizo uwa wanapotea haraka

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad