Watu wanne wameripotiwa kuuawa katika eneo la Bondeni Mpeketoni katika jimbo la Lamu.
Waliotekeleza shambulizi hilo wanadaiwa kuwa wapiganaji wa kundi la Al Shabab ambao walikuwa wamevalia magwanda ya kijeshi.
Walioshuhudia shambulizi hilo wanasema kuwa wapiganaji wao waliwaruhusu waislamu kuondoka huku wale waliokuwa wakristo wakishambuliwa kwa visu na wengine kwa risasi .
Wenyeji wanasema kuwa shambulizi hilo lilitokea mwendo wa saa kumi alfajiri.
Watu wengi waliachwa wakiuguza majeraha.
Nyumba kadha za wenyeji ambao sio waislamu zilichomwa moto.
Operesheni ya uokozi inayoendeshwa na maafisa wa usalama inaendelea katika eneo lililoko karibu na msitu wa Boni ambako inadaiwa wavamizi hao walitorokea.
Hii si mara ya kwanza kwa eneo hilo la Mpeketoni kushambuliwa na wanamgambo wa Al Shabab.
Mwaka 2014 wanamgambo wa Al shabab walishambulia mji wa Mpeketoni na kuua zaidi ta watu 60.
Washukiwa wakuu wa shambulizi hilo la kwanza Mpeketoni walifikishwa mahakamani majuzi na kusomewa mashtaka dhidi yao.
Waislamu nina swali. Mbona mnasema adui yenu ni kafiri na Israel lakini kila siku mnauna wenyewe huko Syria na kwingine kwingi...
ReplyDeleteKila bomu likipigwa mwislamu kapiga mbona makundi yote ya mauaji yanatumia kurani na siyo biblia.... Kila siku kusema dini ya amani lakini wauaji wanasema ni waislamu...
Jibu bila kutukana
Neno la Mungu linasema, lile ninalolipenda sitenda bali lile nichukiayao ndilo nitendalo, ni kwa sababu ya dhambi ndani yangu na neno jema halikai ndani yangu. Ukiona dini au imani inachukia au kumuua mwingine jua kuwa hawana neno jema, ni kuwasidia, kuwaombea na Mungu awahurumie tu
ReplyDelete