Azikwa Kaburini na Kreti za Bia na Soda Kahama

Wakati serikali ikipigia kelele kukemea imani za kishirikina, wilayani Kahama bado ni kitendawili baada ya mkazi mmoja wa Kijiji cha Mwamande, Kata ya Mwanase katika Halmashauri ya Msalala kufariki na baadaye wanakijiji kumzika na mali zake zote yakiwemo makreti ya bia na soda aliyokuwa akiyatumia kwenye biashara yake ya baa.

Tukio hilo limetokea  jana katika kijiji hicho baada ya mwanakijiji huyo, Mahushi Lutaja kufariki na baadaye familia yake kupitisha maadhimio ya kumzika na mali zake zote kwa imani ya kwamba kifo chake kimetokana na kurogwa na wao kuhofia kwamba wakibaki na mali zake nao watakumbwa na mauti.

Kwa mujibu wa diwani wa Kata ya Mwanase, Samson Masanja, Lutaja baada ya kifo chake alizikwa na baisikeli moja vitanda vinne na magodolo yake pamoja na masanduku ya nguo zake zote na vitu vingine vidogovidogo alivyokuwa akivitumia

Pia Masanja alisema, Lutaja alizikwa na makreti ya bia na soda ambayo kabla ya kifo chake alikuwa akiyatumia kwenye biashara yake ya kuuza vinywaji kwenye kijiji hicho cha Mwamande ambapo  tukio hilo limehusishwa na imani za kishirikina

Wakati akiugua ndugu zake waliamini kwamba ugonjwa huo uliopelekea kifo chake ulitokana na kurogwa hivyo familia yake iliingiwa na hofu hiyo hasa kutokana na kuwepo madai ya waganga wa jadi kuamini kwamba ndugu yao alirogwa

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad