Baada ya Bond Kutaka Kujiua Kisa Penzi la Wastara... Wastara Aibuka na Kumpa Masharti Mazito

Staa wa filamu Bongo, Wastara Juma amempa wakati mgumu aliyekuwa mwandani wake ambaye pia ni meneja wake, Bond Bin Suleiman kuwa kama bado anataka waendelee kufanya kazi pamoja asiendekeze wivu baada ya yeye kuolewa.

Wastara aliyeolewa hivi karibuni na Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Sadifa Khamis alisema kuwa ni ukweli usiopinga kwamba yeye na Bond walikuwa wapenzi, kwa kuwa sasa ameolewa na mkataba wake na Bond bado haujaisha imempasa ampe masharti.

“Ninachotaka tuendelee kufanya kazi na azingatie kuniheshimu na kusahau kabisa kama tuliwahi kuwa wapenzi, pia muamuzi wa mwisho ni yeye kama ataona hawezi basi maana nimeshaandaa mtu mwingine,” alisema Wastara.

Chanzo: GPL

Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Huyo Bond achana naye hata kwenye biashara,atajifunza madhara ya usaliti,zaidi sana ukiendelea naye mtajikuta mnajikumbusha malavi davi ya mwanzo,na jinsi ilivyo kwa wanawake wote huwezi kuchomoa.Mumeo atakuwa bungeni,wewe location au kambini na Bond, kuna ndoa hapo au maigizo?

    ReplyDelete
  2. hapo kwenye hiyo picha hamjapendezana kabisa inaonekana huyo shemeji amekaa kitejateja

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad