Baada ya Tarehe ya Uchaguzi Zanzibar Kutangazwa..CUF Watoa Msimamo Wao

Kufuatia tangazo jengine la kihuni lisilozingatia Katiba wala Sheria la Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) Jecha Salim Jecha kutangaza tarehe 20 Machi, 2016 kwamba ni siku ya kile anachokiita uchaguzi wa marudio Zanzibar, Chama Cha Wananchi (CUF) kimeitisha vikao vya juu vya kitaifa vya Chama ili kujadili suala hilo na kutoa msimamo rasmi wa Chama.

Kamati ya Utendaji ya Taifa itakutana Jumatano, tarehe 27 Januari, 2016 na kufuatiwa na Baraza Kuu la Uongozi la Taifa litakalokutana Alkhamis, tarehe 28 Januari, 2016. Vikao hivyo vitafanyika Ofisi Kuu ya Chama, mjini Dar es Salaam.

Chama kinatoa wito na kuwanasihi Wazanzibari wote waliochoshwa na utawala wa kibabe na wa kidikteta wa CCM na ambao walikikataa chama hicho kwa kishindo tarehe 25 Oktoba, 2015 kuendelea kutunza amani na kuwa watulivu katika kipindi hiki kigumu na kusubiri maamuzi ya chama chao wanachokiamini.

HAKI SAWA KWA WOTE

ISMAIL JUSSA
KAIMU MKURUGENZI WA HABARI NA MAWASILIANO
Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Jamani tunaomba amani maana wasiumie wengine wakafaidika wengine

    ReplyDelete
  2. HAO CUF WASHA SHTUKIWA LONG KANA KWAMBA WANATAKA WAARABU WA OMAN ATI WAJE TENA NA KURUHUSU AL QAIDA KUJA WEKA KAMBI YAO HAPO KARIBU ILI KULETA BALAA NA DINI YAO YA KIISLAMA ,HAMPATI NAFASI KAMWE,

    TANZANIA ILIKUWA IMETULIA KWA MIAKA NA KWA NINI SASA NDIO MNATAKA MUYABADILISHE MAISHA KWA UBADHILIFU WA SHERIA NINYI MNAFIKIRI TANZANIA IMELELE= NEVER HATA MUENDE WAPI HAKUNA NO NO NO CUF ZANZIBAR MSITULETEE NUKSI KATIKA MUUNGANO WETU ULIOKUWA UMENAWIRI SASA MNATAKA KUTURUDISHA NYUMA KARNE YA 18.

    SASA KUMUANDIKIA PAPA POUL NGIYO IWEJE YULE SIO MWANA SIASA TULE NI MTU WA DINI .NA TOYE HIO NI SABABU YA KUONGOZWA NA VIONGOZI WASIOKUWA NA ELIMU YA KUTOSHA, KWA NINI MSIMWANGIKIE MUFTI WA OMAN AKAJA INGILIA SWALA LENU. THATS A BIG MISTAKE MMEFANYA. HAPO KUNA AU KWA NINI MSIANZIE HAPO KABLA HAMJAENDA KWA WAZUNGU= NA WAZUNGU WENYEWE WAKRISTU WAKATI NYIE WAISLAMM HAILETI MANTIC AT ALL,

    SHAME ON YOU CUF

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad