Balozi Amina Salum Ali Amuomba Seif Sharif Hamad Kufikiria Upya Uamuzi Wa Kususia Uchaguzi Wa Marudio Zanzibar

Balozi Amina Salum Ali
Kada aliyegombea urais kwa tiketi ya CCM, Amina Salum Ali amesema mgogoro wa kisiasa Zanzibar hautakwisha hata baada ya Uchaguzi wa marudio kwa kuwa ni wa kihistoria na baadhi ya viongozi hawana nia ya dhati ya kuendeleza Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) visiwani humo.

Balozi Amina pia amesema uamuzi wa CUF kususia uchaguzi wa marudio visiwani humo utasababisha mpasuko mkubwa zaidi na kumtaka katibu mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad kufikiria upya na kubadili msimamo huo kwa faida ya Wazanzibari wote.

Zanzibar imekuwa ikikumbwa na mgogoro wa kisiasa kila inapoingia kwenye Uchaguzi Mkuu kuanzia mwaka 1995 baada ya vyama vya upinzani kuruhusiwa, na vurugu za mwaka 2005 zililazimisha CUF na CCM kuingia kwenye mazungumzo yaliyozaa SUK.

Lakini dalili za SUK kuendelea sasa zinaonekana kufifia baada ya CUF kupinga uamuzi wa mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha wa kufuta matokeo ya uchaguzi wa rais wa, wawakilishi na madiwani visiwani humo Oktoba 28, mwaka jana na kutangaza uchaguzi mpya Machi 20, ambao chama hicho kikuu cha upinzani kimesema hakitashiriki.

Balozi Amina anaona kuyumba kwa Serikali hiyo ya umoja wa kitaifa kunatokana na Maalim Seif kutotambua kuwa maridhiano hutokana na kupata kitu fulani na wakati huohuo kukubali kupoteza kingine.

“Mimi namshauri Seif kujua kuwa katika uchaguzi kuna kushinda na kushindwa, afahamu kuwa Tanzania itajengwa na Watanzania na kwa upande wa Zanzibar, Wazanzibari wanataka maendeleo,” alisema.

“Seif analalamika wakati yuko serikalini, anakutana na mwenzake (Dk Shein) wanakula haluwa na kufurahi pamoja, lakini akitoka nje, anageuka. Tutafika wapi kwa siasa za namna hii?”

Amina alisema Zanzibar ilikuwa na bahati kumpata Dk Shein ambaye Maalim Seif angeweza kumtumia kufanya mambo anayotaka, lakini ameshindwa kugundua fursa hiyo na kuanza kujivuruga.

“Chini ya Dk Shein, Zanzibar imepata fursa nzuri ya kufikia maelewano. Shein anawawakilisha Wazanzibari wote na anajua siasa za Zanzibar ni mstahamilivu, ni mwenye busara, msomi na mpenda maendeleo,” alisema Balozi Amina na kuongeza kuwa:

“Hivyo huu ulikuwa wakati mzuri kwa Seif kushirikiana wafanye anachotaka kwa ajili ya maendeleo ya Wazanzibari.”

Alisema kitendo cha CUF kususia uchaguzi wa marudio kitaongeza mpasuko wa kisiasa badala ya kuupunguza, hivyo ni vyema Seif akaliangalia hilo vizuri na kubadili msimamo huo kwa faida ya Wazanzibari wote.

“Uchaguzi huu wa marudio ndio utakuwa kipimo cha kuonyesha nani anakubalika Zanzibar sasa Seif akisusa maana yake nini?” alihoji.
Tags

Post a Comment

9 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. danganya toto Bi dada Amina, badala ya kuokoa maisha ya wazanzibari na kumpa nasiha dr. Ali Shein pia awe anafanya uadilifu badala yake mnahimiza subira zisizo na mwisho upande mmoja mkisahau kuhatarisha maisha ya watu na mali zao kwani kila mtu hivi sasa anafikiria kivyake kuhusu jambo hili nchi yenyewe masikini watu pia masikini na halafu mnalizimisha jambo ambalo haliwezekani sio kuwa mimi ni mpenzi wa cuf ila ni mpenzi wa watu na maisha yao na mali zao ukizungumzia subra mimi nafikiri cuf wamewasubiria ccm si zaidi ya mara moja lakini hao ccm hawawasubirii cuf hata mara moja jee mpaka lini mambo haya yataendelea au mtaendelea na kauli ya asha bakari hamtoi serikali kwa karatasi kwani hii ni serikali ya kimapinduzi kama wengine wanavyo iita ya kivamizi ya John okello na Nyerere na wamakonde wake wa sakura kwaheri ukoloni karibu mkoloni mweusi na acheni ubaguzi wa kuwabagua watu kwa rangi zao kama mnavyo andika katika mabango yenu hii nchi si ya machotara ni ya watu weusi jee hao weusi na weupe wameumbwa na nani ? acheni mambo hayo yamepitwa na wakati msiogope ufakiri na alhali hamtaki kurekebisha behaivour na attatude zenu, chuki zenu zitawafikisha pabaya.

    ReplyDelete
  2. Mtu mzima ovyo shut up your shit muoth.

    ReplyDelete
  3. Nw sasa ni mda wa Shein na CCM kutumia busara kama vle ambavyo Maalin Seif na CUF ilivyokubali alivyokubali kuingia kwnye mazungumzo. Ni lini CCM watatumia busara? Kauli ngap za kichochez wamezitamka wamezionyesha na kuzifanya? Yote hayo hawazungumzi utasikia wanasema ni propaganda za kisiasa tu et kua siasa za zanzibar zinamatan mengi. lakina wakifanya upande wa pili huku nia makosa tna mengine yaundiwa sababu hadi yakapelekea futwa kwa uchaguz illegely.Nw ni mda wa kutoa tathim ya zanzibar kama mtanzania na c kama kada wa chama fulan tumeona kauli nying za makada wa CCM wakiongea kichama zaidi kuliko kiutaifa katika swala hili na hyu mama nae kaelekea upande ule ule. MaalimSeif na CUF wameshatumia busara saaana kumbuken kuchoka kupo, huu ni wakati muafaka sasa wa Shein n CCM watumie busara na c Maalim na CUF kwa kua wao ndo wanaweza tengua hali hii mbaya ya kisiasa na wasipeleke lawama kwa CUF.

    ReplyDelete
  4. Wanasema charity starts at home... Nadhani ingekuwa vyema ungeanza kwanza kukishauri chama chako kirekebishe pale kinapokosea na Cuf pia kama kinakosea kirekebishe pale kinapokosea kwa maslahi mapana ya wananchi wa Zanzibar! Madaraka tutayaacha hapa duniani lakini tukumbuke if anything happens tutaenda kuwajibika kwa Mwenyezi Mungu! Duniani tunapita tu siasa zisitawale sana vichwa vyetu hadi tusahau kuna Mungu ambaye anaona kila kinachoendelea kwa dhahiri na kwa yaliyojificha pia! Ee Mwenyezi Mungu endelea kuisimamia Zanzibar kipindi hichi kipite kwa amani na utulivu

    ReplyDelete
  5. Hiyo kawaida yenu Cuf. Museme nyinyi na mukiambiwa ukweli munakuja juu tena na matusi. Jibuni hoja, otherwise shut up waacheni wahusika wafanye kazi. Kwani hao CCM hawajawachoka na vurugu na kila siku kuwa victim ni nyinyi tu. Kwani hamna watu wengine wenye mali zao isipokua nyinyi tu. Jibuni hoja na Maalim hatakiwi. Mbona wenzenu ukawa wamebadili kandidet na wakapata support kubwa mno. Weka Babu Duni muone kama hamtapata support na hiyo haki munosema. Cha kushangaza muungano hamuutaki lakini mbio munaenda huko huko bara kutoa conference zenu. Hiyo ni double face.

    ReplyDelete
  6. Shangingi lilobebwa kama migiro
    Wakafuzwa kazi kwa kutojuwa kazi

    ReplyDelete
  7. Huyo bibi ni mjinga tu, kwa nini anamkandamiza Seif tu?? Basi na Shein pia alegeze kdgo kupitia Jecha ili mshindi halali atangazwe, mbona hataki km kweli mnataka usawa na democrasia kufuatwa?

    ReplyDelete
  8. kikubwa hapa tuombe Mungu viongozi wetu wakae mezani waje na majibu mazuri wasitofauiane.Vita sio kitu cha kuzungumzia jamani tunaomba viongozi wetu Mungu awaongoze msisikilize wanaochochea uadui kati yenu. Mungu ibariki Tanzania.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad