Bavicha Wataka Chama Cha Mapinduzi Kifutiwe Usajili Kwa Kuwa Kimeonyesha Ubaguzi wa Rangi Zanzibar

Baraza la Viajana wa Chadema (Bavicha)  limemtaka msajili wa vyama vya siasa nchini kutoa tamko kuhusu vitendo vya ubaguzi wa rangi vilivyooneshwa na baadhi ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakati wa sherehe za maadhimisho ya Mapinzuzi ya Zanzibar.

Akiongea na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Katibu Mwenezi wa Bavicha, Edward Simbeye alisema kuwa kutokana na vitendo hivyo vya kibaguzi, msajili anapaswa kuchukua hatua kwa mujibu wa sheria ikiwa ni pamoja na kuifutia usajili CCM.

“Sheria ya usajili wa vyama vya siasa iko wazi. Sheria ya usajili wa vyama vya siasa inasema, chama chochote kitakachofanya siasa za kibaguzi huenda wa kikabila, kidini ama vinginevyo chama hicho kitafutwa. Tunataka kauli ya msajili wa vyama vya siasa. Ni lini, wakati gani ataifuta CCM,”alisema Simbeye.

Simbeye alisema kuwa Baraza hilo la vijana la Chadema linamtaka msajili kutoa tamko lake ndani ya kipindi cha siku tatu na kwamba asipofanya hivyo, watachukua hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kwenda mahakamani.

“Msajili wa vyama vya siasa atuambie ni lini sheria hiyo imeondolewa mpaka leo CCM ni chama cha siasa kwenye taifa hili. Vinginevyo, ndugu waandishi wa habari tumepanga… na haya ndio maazimio ya vuguvugu hili, tutampeleka mahakani,”alisema.

Wakati hayo yakiendelea, uongozi wa CCM ulitoa tamko na kuomba radhi kwa vitendo vya kibaguzi vilivyojitokeza kwenye sherehe hizo ambavyo vilifanywa na kundi la watu wanaoaminika kuwa ni wafuasi wa chama hicho. Watu hao walibeba bango lenye ujumbe wa kibaguzi.

Tags

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kwani ubaguzi gani huo mnaousema Bavicha?nyie mnataka siasa za maji taka kwa muonekano halisi, kama siyo ubaguzi nani anaweza kwenda Arusha au Kilimanjaro ambae si mwenyeji na mzaliwa huko atapewa hata ujumbe wa nyumba kumi? nyie ndo mlitakiwa kufutwa mapema kwa sera zenu za ukanda ambazo bado zitaendelea kuwatafuna. Kweli kwa jambo lile huko znz ni makosa lakini msemacho Bavicha mmechemsha kwanza anzieni kwenu kwani nyie imekuwa ni kansa itawamalizeni.

    ReplyDelete
  2. Kama kufutwa, ifutwe chadema kwa siasa zake za kikabila na kidini, mmejazana watu wa kaskazini na walutheri kibao, mpaka huyo FISADI wenu akapiga kampeni kanisani Tabora na mkewe akawahamasisha wachaga wachague chadema, hamkusema chochote, yawenzenu midomo juu....hovyooo

    ReplyDelete
  3. Eti CCM ifutwe!! Mnaihofia sio, mnaiogopa ndio?? hahahaha

    ReplyDelete
  4. Kusema Zanzibar ni nchi ya waafrica ni ubaguzi au ukweli?
    Upuuzi huo upo Tanzania tu mtu akiwa maji ya kunde kidogo basi yeye si mwafrika, yeye ni mwarabu, yeye ni tofauti na watanzania wengine? Mtu kujisifia kuwa yeye ni mwarabu kwake yeye anaona big deal.Kwa kipindi kirefu hao wanaojiita warabu wa Zanzibar wamekuwa na madai ya vkipuuzi ya kutaka nchi yao leo wanatokezea watu na kuwaambia ukweli ati ubaguzi?

    ReplyDelete
  5. HAPO CCM LAZIMA IFUTWE TU IKIWA FIFA INAFUNGIA WACHEZAJI KWA NINI CCM ISIFUTWE

    ReplyDelete
  6. HAPO CCM LAZIMA IFUTWE TU IKIWA FIFA INAFUNGIA WACHEZAJI KWA NINI CCM ISIFUTWE

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad