Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe amepinga uamuzi wa kufutwa kwa matokeo yote ya uchaguzi visiwani Zanzibar
Amesema inashangaza kuona uchaguzi ulifutwa kwenye majimbo yote, badala ya yale yaliyokuwa na matatizo tu “Kilichotokea Zanzibar kimeihuzunisha dunia,” alisema mbunge huyo wa zamani wa Mtama mkoani Lindi. “Watanzania waelewe, kilichoishitua dunia ni kule kufuta matokeo kwa ujumla wake.
Yaani majimbo yote hakuna hata moja lililofanya vizuri? Hapa ndipo tunapata kigugumizi. Sasa tunakwenda wapi, tunafanya kitu gani? “Ilitakiwa kuwe na ubaguzi; majimbo mawili, matatu, manne, matano, haya hayajafanya vizuri ndiyo uchaguzi urudiwe. Kaubaguzi kale kangewekwa, hiyo ingefanana na sura ya dunia ya haki.
Bernard Membe Akosoa Vikali Uamuzi wa Kufutwa Kwa Matokeo yote ya Uchaguzi Zanzibar..Adai Dunia Imehuzunika
3
January 23, 2016
Tags
Huyu membe cijui kawa mende na akili za chooni, kisiasa anaanza kupotea kwa uropokaji usio na faida kaanza na serikali ya JPM, now la uchaguzi cku zote alikua wapi, Hana jipya anatafuta kiki kwa jpm hapa kazi 2.
ReplyDeleteKweli Membe
ReplyDeleteHama CCM basi
ASISEME UKWELI,UKWELI UNAUMA EEE BASI KULENI MWANI KWA WINGI MVIMBIWE MPUNGUZE JAZBA ZENU ZA KISHETANI.MEMBE SI KAMA NYINYI VIBAKA WA SIASA,ANAIJUA DUNIA,ANA MAWASILIANO NA DUNIA NZIMA.SASA UNATAKA KUMZUIA ASISEME.SIYO YEYE NI DUNIA INAYOTULALAMIKIA.CCM IMETIA DOA NA FEDHEHA KUU ZANZIBAR.HILI HALITASAHAULIKA.MAREKANI WANALAANI, VIVYO HIVYO MATAIFA YA CANADA,BRAZIL,ARGENTINA,UFARANSA,URENO,SPAIN,PORTUGAL,SWITZELAND,LUXEMBOURG,GERMANY,SWEDEN,DENMARK,FINLAND,POLAND,ITALY,GREECE,RUSSIA,JAPAN,AUSTRALIA, HAPA NI KWA UCHACHE WAMEENDELEA KULAANI NA KUIBEZA CCM KUWA NI SHAMELESS DICTATORS KWENYE DUNIA YA LEO ILIYOSHEHENI WAKWELI,WAWAZI NA WASTAARABU.MEMBE ASISEME UKWELI UNAFIKIRI YEYE NI MSHAMBA KAMA NYINYI MABUNDA YA WANAFIKI MNAOLIPWA KWA KUSHABIKIA MAOVU?NA MLAANIWE CCM MPAKA KHIAMA.
ReplyDelete