Biashara Zinazotumia Mfumo wa Network Marketing na Ulaghai Uliofichwa Ndani yake

Mara nyingi tumekua tukiona au kukutana na watu au ndugu zetu wanaojiita wawakilishi wakijaribu kutushawishi kuingia katika kile wanachokiita biashara zenye mafanikio, ambapo wanatushawishi kujiunga na kampuni inayouza bidhaa zake kwa mfumo wa Network Marketing au Multi-Level Marketing (MLM). Katika mfumo huu unapata commission na faida kwa kuingiza watu wengine wanunue bidhaa husika na faida yako itaendelea kua kubwa kama na wao watashawishi watu wengine wajiunge katika msururu huu. Makampuni haya kwa hapa Tanzania yapo mengi wakiuza bidhaa kama za Aloevera, Kahawa zenye mchanganyiko wa Garnodema n.k.

Naomba itambulike kua Lengo la uzi huu sio kukosoa kampuni yeyote ile, bali ni kueleza na kuelimisha umma athari za mfumo wa kilaghai unaotumika katika biashara za namna hiyo

Kabla sijaamua kuandika uzi huu nimekua nikiona watu wengi wakidanganyika na kuingizwa mkenge kwenye biashara hizi aidha kwa kutokujua ama kuingizwa tamaa kwa ushawishi wa wawakilishi hawa ambao wanakua na vipeperushi vinavyotoa maelezo ya biashara huku vikionyesha baadhi ya watu waliofanikiwa katika mfumo huu wakiwa katika picha na Magari Mazuri na Majumba ya Kifahari.

Network Marketing au MLM ni mfumo unaofanya kazi kwa Idea kwamba unauza bidhaa kwa watui ambao nao watauza bidhaa kwa watu ambao nao watiuza. Mfumo huu kamwe hauwezi kusemwa kua ni mpya kwenye masoko ili upate msamaha wa kutokuhusianishwa na kanuni na taratibu za kawaida za Marketing katika uuzaji na ununuzi wa bidhaa. Mfumo huu una ulaghai wa hali ya juu na kiuhalisia Mfumo mzima hauna faida hasa kwa watu wa chini, na sio sustainable kwa muda mrefu - in reality the system ‘is designed to fail” 

Swali ambalo ningependa ujiulize ni hili; Kama bidhaa husika ni nzuri sana na inahitajika katika jamii kama wanavyoinadi, kwanini wasitumie mfumo wa kawaida wa masoko ambao umeinufaisha dunia nzima tangu karne?. Jambo la kwanza kabisa ambalo mtu yeyote lazima alielewe ni hili; Katika biashara yeyote swala la demand and supply au kwa Kiswahili Ugavi na mahitaji lazima lizingatiwe na kama ukakosea ukafanya makadirio ya chini au ya juu sana katika kimojawapo kati ya hivyo basi hakuna mafanikio yeyote yatakayo patikana katika biashara utakayoianzisha. MLM nyingi zinaoverestimate supply and demand kwa kiwango cha juu sana, Na tatizo kubwa hapa ni la kutokutumia akili ya kawaida kabisa; Kivipi sasa?.

Chukulia mfano huu; Tuseme wewe ni mwakilishi wa mojawapo ya makampuni haya na ukaweza kuwashawishi wenzio (wauzaji) kumi ukapata commission na faida kiasi ambao watadhamini kumi na wao kudhamini wengine kumi kila mmoja, mpaka kufikia kizazi cha tatu utakua na idadi ya watu 1000, na hapo utakua umeumaliza mtaa wako. Kufikia kizazi cha sita utakua umefikisha watu 1,000,000 na huo utakua ni mkoa mzima tayari na kila mmoja katika hawa akiamini katika mafanikio yatakayotokana na uuzaji wa bidhaa husika, lakini watamuuzia nani sasa na kila mmoja ni muuzaji?. Kwenye vikao vyao utawasikia “Kila mmoja hapa anaweza, hii ni fursa ya maisha, angalia mahesabu utaniamini”, ila Jaribu kuongelea kuhusu oversaturation ya soko na hasara itakayosababishwa nayo utawasikia wakikuambia “sio kwako bwana mafanikio haitatokea hivyo kwako nayaona mafanikio yako hata nikikuangalia machoni”. Tumia akili ya kawaida utapata jibu kuhusu hilo.

Network Marketing ni mfumo wa kiunyonyaji katika mahusianao ya mtu na Kama uko katika biashara hii lazima ukubali kumeza ukweli mgumu kwamba biashara yako inakua kutokana na exploitation of personal relationships. Baada ya kuingia katika biashara hii, marafiki na ndugu zako wanakua ni wateja wako, sasa jiulize uko tayari kumwingiza Mama yako kwenye huu mfumo wa wizi ukijua hakuna faida kubwa mbeleni?

Kufeli kwa biashara yeyote ile kunaumiza sana, ila kwa biashara yeyote ndogo kunakuwepo japo nafasi ya kufanikiwa. Nafasi hiyo ndogo ya mafanikio kamwe haipo kwenye MLM labda kama faida inayotokana na kushindwa kwa wengine utaitafsiri kama mafanikio.

By Bill The Goat/ JF

Tags

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mmmmh mi napita Tu...

    ReplyDelete
  2. Mhhhhhhh naomba unitafute 0656781501 huenda wewe ndo hujui

    ReplyDelete
  3. Umenifumbua leo leo ilikuwa kidogo nipigwe

    ReplyDelete
  4. Mi nazani ungali washawishi watu kutafuta network marketing ya uhakika kuliko kuwapoyeza kabisa
    Alafu ungesoma kidogo mult level marketing ni mfumo uliopitwa na wakati miaka mingi iliopita sasa hii network ya sasa nintofauti na unayowashawishi watu wasiingie mie nazani ungefany utafiti kabla hujazungumza kupitia page so I sory

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad