BIFU la Wanamuziki Diamond na Ali Kiba Lafika Pabaya

DAR ES SALAAM! Kutokana na mwenendo wa bifu lao la chini kwa chini ni dhahiri mafahari wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platmumz’ na Ali Saleh Kiba ‘King Kiba’ wamefika pabaya kwani safari hii zimeibuka tuhuma za kuzibiana riziki kimataifa, Ijumaa Wikienda linashuka na mchapo kamili.

Chanzo makini kimeeleza kuwa, Team Kiba ambao umoja wao unaonekana zaidi katika Mtandao wa Instagram, wamecharuka vibaya wakimtuhumu Diamond kuwa anawasiliana na vituo vya kimataifa kama MTV na kuwaambia wasipige nyimbo za King Kiba.

“Jamaa hafanyi fea, anawasiliana na wale wa vituo vya kimataifa na kuwaambia wasipige nyimbo za Kiba, anamzoofisha kweli,” kilimwaga ubuyu chanzo chetu.

Mara baada ya kusambaa kwa taarifa hizo za Diamond ‘kumficha’ mwenzake kimataifa, Team Kiba na Team Diamond walianza kuporomosheana matusi mazito mtandaoni.

Team Kiba waliapa kufanya ziara nchi nzima kushinikiza Diamond aache ubaguzi huku Team Diamond wakimtetea msanii wao wakisema si kweli kwamba anafanya hivyo bali amekuwa akiwasaidia wasanii wengi hivyo Team Kiba wanatapatapa.

Baada ya ubuyu huo kutua mezani, mwanahabari wetu alimsaka King Kiba kupitia simu yake ya mkononi ambapo alisema kama kweli vituo hivyo vinamsikiliza Diamond, vitakuwa havimtendei haki.

“Kama kweli MTV watakuwa wanampatia jukumu Diamond la kupitisha ngoma zetu basi watakuwa hawafanyi fea, sidhani kama ni kweli wanafanya hivyo na Diamond anaweza kufanya hivyo,” alisema Kiba.

Akijibu tuhuma hizo mwishoni mwa wiki iliyopita Diamond alikaririwa katika Televisheni ya Taifa (TBC 1), akielezea namna ambavyo amekuwa akisikitishwa na watu kumwambia anawabania baadhi ya wasanii kupigwa kimataifa na kusema wanamuonea.

Source: Global Publishers

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. ACHENI UJINGA SASA DIAMOND ANAUWEZO GANI WA KUZUIA MTV WASIPIGE NYIMBO ZA MSANII FURANI KWANI DIAMOND YEYE KAMA NANI MTV

    ReplyDelete
  2. NDO ALIVYOSEMA MWENYEWE DIAMOND YA KUWA MTV WANAMUULIZA KILA MSANII ANAETAKA KUPIGIWA NYIMBO. SO KAMA NI MJINGA NI DAI.

    ReplyDelete
  3. Enter your comment...achene kuwawajaza chuki mioyon mwao hao wasanii uchochezi huo ndio maana tanzania haiyendelei maana mtu akipiga hatua wajinga wanamrudisha nyuma

    ReplyDelete
  4. Na huyo daimond huwo mwili Ni gym tupu au kuna vitu vyengine asijaribu vina haribu nguvu za kiume ....napita tuuu.

    ReplyDelete
  5. Kwanza mapacha hao hawana ugomvi kabisa ila vyombo vya habari vinawagonganisha kiaina ili viuze

    KIGOMA MOJA, DAR MOJA NA TZ MOJA

    ReplyDelete
  6. OK TULIENI NYOTE. KAMA MNATAKA USHAHIDI WA KWELI NTAFUTEN MM, NIWAELEZE KINAGA UBAGA

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad