Bosi wa TP Mazembe Asalimu Amri Kwa Samatta..Huu Ndio Uamuzi Alioutoa

HATIMAYE mmiliki wa klabu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Moise Katumbi amekubali mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta kujiunga na KRC Genk ya Ligi Kuu ya Ubelgiji.

Mchezaji huyo alitarajia kurejea jana nchini kwa ajili ya safari ya Ubelgiji kwenda kuanza maisha mapya katika soka la Ulaya.

Samatta tayari amekwishasaini mkataba wa awali na Genk wa miaka minne na sasa anakwenda kukamilisha taratibu zilizobaki.

Samatta na Genk wanataka kukimbizana na muda ili kuwahi kabla ya kufungwa kwa dirisha dogo la usajili.

Meneja wa Samatta, Jamal Kisongo alisema kuwa hatimaye Katumbi ameridhia Samatta aende klabu anayoipenda ili kuendeleza soka lake.

Katumbi alikuwa anataka Samatta aende Nantes ya Ufaransa, ili kucheza soka huko, lakini mchezaji huyo hakupenda kwenda huko na alikuwa tayari kubaki Congo kumalizia mkataba wake unaomalizika Aprili.

Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Usilete scandali tuu
    Pesa mbaya

    ReplyDelete
  2. ANAUJUA MPIRA SAMATTA,KIWANGO CHAKE NI CHA LIGI KUBWA ZA BARA LA ULAYA.HATAKAA UBELIGIJI SAMATTA,WATAMUONA NA,WATAMWITA SPAIN,ITALY NA ENGLAND.NI MCHEZAJI MKUBWA SANA SAMATTA.ANA AKILI YA ZIADA YA UTAFUTAJI MAGOLI.ANAWAPUMBAZA MABEKI KWA KUTUMIA SAIKOLOJIA-ZIADA,HAPA TANZANIA ALIWAHI KUTOKEA MCHEZAJI MMOJA TUU MAREHEMU MAFISANGO.LA PILI SAMATTA HANA UGENI NA EURO NA DOLA,CHENJI NZITO TAYARI ANAYO SAMATTA,KESHAONYESHA SI LIMBUKENI WA NGAWIRA NZITO,HIVYO NI DHAHILI KULE ULAYA,ATATENGEMAA.WELLKOMEN JUGGLER SAMATIA-GOOOOLI.NI GOLI WASIKILIZAJI!

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad