Breaking News: Jeshi la Polis Lafanikiwa Kukamata Wafanyabiashara Wakongwe wa Madawa ya Kulevya

Jeshi la Polisi kanda maalum ya Dar es Salaam, limefanikiwa kuwanasa wafanyabiashara wakongwe wa dawa za kulevya nchini ambao pia wanadaiwa kufanya biashara haramu za binadamu ambao wamekuwa wakiwasafirisha kutoka nchini kwenda katika nchi zinazozalisha dawa za kulevya.
Magwiji hao wa dawa za kulevya nchini waliotiwa nguvuni na jeshi la polisi ni pamoja na Mohamed Abdallah Omary, Nassoro Suleiman na  meneja wa duka la Tungwe Bureau de Change ambalo hutumika kusafirisha fedha za dawa za kulevya kwenda nchini Pakstani kinyume na sheria.
Taarifa hiyo kamanda Sirro, amesema kwasasa jeshi la polisi limejipanga kuhakikisha linadhibiti mianya yote ya dawa za kulevya ambapo pia katika msako mkali uliofanyika mwishoni mwa wiki gari zenye namba za usajili T271 DCT, T916 DCL, T593 CEL na T999 DDB  zimekamatwa.
Kamanda Sirro amesema kuwa kumeibuka wimbi la wafanyabiashara wa dawa za kulevya kusafirisha watanzania kuwapeleka nchini Pakstani na kuwaacha kama bondi ili wapatiwe mzigo mkubwa wa dawa za kulevya ambapo wengi wao wamekuwa wakiuawa ambapo amesema jeshi limejipanga kusambaratisha mtandao huo.

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mmmmh,ngoja tuone mwisho wake.kila la heri.

    ReplyDelete
  2. SASA NINYI NI KUSHIKA TU WATU BILA EVIDENCE?BASI KILA KIJANA ATAKUWA MTU WA

    SEMBE UNLESS ANAFANYA BANDARINI AU TRA, KAMA ZITAKUWA ZINASIKILIZWA

    KELELE ZA WATU AMBAO WANA MABEEF NA WENGINE NA KUBAMBIKIWAWA, TU HAYA

    MTAONA MWISHO WAKE.

    SIKU ZOTE POLISI ILIKUWA WAPI ?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kwa nini kila siku,kila kona ya Tanzania watajwe haohao tu?
      Umeshawahi kusikia Mengi,Baharesa,manji na wengine wengi wanahusishwa na dawa za kulevya.

      Delete
  3. Enter waTz ss n vigeugeu akishikwa ooh,hakuna ecodence,wakiachwa polis wako wap acha ungese ww,jiulize kwa nini hujakamatwa ww,au n baba yako nn? please stop senging

    ReplyDelete
  4. Unanyosolewa wewe si bure.
    Au na wewe ni muhusika wa madawa ya kulevya?

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad