WAMILIKI wa Taasisi za Kifedha wanatakiwa kujiridhisha kama waajiliwa katika taasisi hizo kama wanahusika kwa njia moja ama nyingine katika uharifu unaohatarisha maisha ya wakazi wa jijini la Dar es Salaam.
Hayo yamesemwa na Kamanda wa Polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za makao makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar es Salaam leo.
Kamanda Sirro amesema kuwa hatua za makusudi zimechukuliwa katika maeneo mbalimbali hasa ya eneo la Kibiashara la Mlimani City kutokana na matukio mengi ya uporaji wa fedha kwa kutumia pikipiki.
Pia amesema kuwa pamoja na sheria hizo kuchukuliwa watafanya operasheni maalumu katika eneo hilo na kutafuta namna nzuri ya kuondoa pikipiki katika maeneo hayo.
Katika Operasheni zilizofanywa na Jeshi hilo wamefanikiwa kuwakamata majambazi nane pamoja na kumamata Bunduki mbili aina ya Pump Action ambazo namba zake zilifutwa na kukatwa Mtutu.
Aidha Kamanda Sirro amesema kuwa katika Operasheni hiyo wamemkamata jambazi aliyekuwa akitafutwa kwa muda mrefu anayejulikana kama Mkama Hassan mkazi wa Gomgolamboto jijini Dar es Salaam na alipopekuliwa alikutwa na Bastola aina ya Chinese iliyofutwa
Udaku Special Blog
.