Breaking News:Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Apewa Masaa 48 Ya Kujieleza

NAIBU Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais ( Mazingira na Muungano) Luhaga Mpina amempatia saa 48 Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo kujieleza sababu za Jiji la Mwanza kuwa chafu.

Mpina alisema hayo jana jijini hapa wakati akieleza mambo aliyoyabaini wakati wa ziara yake ya siku mbili jijini Mwanza.

Alisema licha ya serikali kutangaza suala la usafi kuwa ni hoja ya kitaifa, Jiji la Mwanza linatisha kwa uchafu wa mazingira.

Mpina ambaye alianza ziara jana kukagua maeneo mbalimbali ya jiji, alisema uchafu wa jiji kwa kiwango kikubwa unachangiwa na baadhi ya watendaji wa Serikali na wataalamu, kutowajibika vyema.

“ Ni sehemu ndogo tu ya uchafu wa jiji la Mwanza unaochangiwa na wananchi, kutokana na hali hii nilivyoiona ninampatia Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo masaa 48 ajieleze ni kwanini jiji la Mwanza ni chafu ilihali lina watendaji wa kutosha na wataalamu”, alisema.

Alisema Januari 30 mwaka huu atarudi jijini Mwanza, kushiriki usafi na wananchi kama sehemu ya kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano.

Udaku Special Blog
Tags

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kumbe naibu waziri bossi WA mkuu WA mkoa makubwa haya
    Poleni madc Na wakuu wa mikoa

    ReplyDelete
    Replies
    1. Watapokea amri kwa watoto waliowazaa Na kuwanya wima
      Kisa Hapa kazi fyuuuuuuuu
      Wavimbieni wasitake sifa
      Kama wao wameteuliwa rais hata nyinyi wa kuu mikoa Na mnaapishwana rais Kama wao

      Delete
  2. NDUGUZAGU WA CCM MWANACHAMA MWEZETU AKIWA NI RAIS WETU MAKUFUA ANAPOTEZA DIRA YA CHAMA TOKA AIGIYE WARAIS YEYE NIBADARI MAPATO MAMBOMEGINE KAYASAHA PIYA KASAHAU KWAMBA CHAMA NDICHO KILICHO MUWEKA KITINI WATU WANACHUKUWA UMEYA YEYE YUKOWAPI KASAHAU KIKWETE ASIGE IMARISHA CHAMA NAKUTHABITI SEHEMUYA MUHIMU TUSIGEPATAURAIS

    ReplyDelete
  3. oma hueleweki na comment yako.

    ReplyDelete
  4. sasa wewe mdau Oma, ulitaka magufuli afanyeje wakati idadi ya madiwani ccm huko wanakogombea umeya ni ndogo kuliko upinzani au ulitaka akakuchakachulie, hehehehehee! unaloloma tu. acha rais afanye kazi bwana ya chama badae, kwanza alichaguliwa na watu wote sio na chama. mjipange kivyenu

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad