Aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Leticia Nyerere amefariki dunia katika hospitali ya Doctors Community iliyopo Lan ham, Maryland jana saa mbili usiku kwa saa za Afrika Mashariki..
Leticia aliolewa kisha kutengana na mtoto wa Hayati Baba wa Taifa, Madaraka Nyerere mwaka 1996, ambapo walifanikiwa kupata watoto watatu.
Leticia alikuwa mtoto wa Mzee Musobi Mageni. Julai 27 2015, Leticia alitangaza kuihama CHADEMA na kurejea Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Mungu ailaze roho ua Marehemu mahali pema peponi,
Amina
Jamani kilichomuuwa huyu Dada ni kitu gani?? Mbona hatuelezwi......ndio tunajua alikuwa amelazwa lakini je alikuwa anasumbuliwa na maradhi gani????.....Waandishi wa habari wa Nchi hii ni majanga kha!!!!!
ReplyDeleteUkijuwa anaumwa nini utamfufuawa
DeleteKama ulipita jiandaye baby wewe
Jamani kilichomuuwa huyu Dada ni kitu gani?? Mbona hatuelezwi......ndio tunajua alikuwa amelazwa lakini je alikuwa anasumbuliwa na maradhi gani????.....Waandishi wa habari wa Nchi hii ni majanga kha!!!!!
ReplyDeleteUlipita Kwani hapo
DeleteJiandaye Na wewe ndo habari ya mujini
Point of correction,,,,sio mtoto wake ni Mkwe wake,,,,R.I.P Leticia.
ReplyDeleteMakongoro sema wagonjwa unao bado madaraka , Rosemary , na hata Anna wanatisha
ReplyDeleteRIP Leticia
Ila shemeji akome kuita watu wagonjwa
Kwanza kabisa poleni kwa msiba
ReplyDeleteLakini najuuliza nimeona kwenye vyombo vya habari eti gharama za kusafirisha mwili wa marehemu zitagharamikiwa Na serikali , ni kigezo kipi hapa kimetumika
Niyuavyo mimi mfanyakazi wa hurusiwa mke na watoto wanne , pamoja baba Na mama WA pande zote mbili,
Serikali toka awamu ya tatu imekuwa ikigharamia family ya Mwl, lakini ni mkwewe tu ndiyo kugharamikiwa gharama hizi, kwa hesima zote mama WA watu hana makuu nafikiri hata watoto wake pia, tulisikia kuna bima za maisha hata kwa Watanzania waiishio ughaibuni
Marehemu nadhani Kabisa alikuwa na bima hii,
Au tu kwa sababu alihama chadema kuhamia CCM
Haniingilii kichwani kwa hili la kugharamia gharama hizi
Kama mchango basi utoke CCM, chadema Na watu binafsi
Kwa sababu wako watu wamekufa kwa bomoa bomoa ya msimbazi hadi leo hatujaona ikulu kwenda kuwapa pole je hawa siwatu? Ambao mauwaji yao yamesabaishwa na serikali?
Tuwe wakweli tusibaguwane kwenye matumizi ya fedha za serikali
Ya Zanzibar mpaka leo kitendawili
Kana kwamba hakuna lolote
Mungu ibariki Tanzania
Pumzika kwa Amani dada Leticia