Breaking News;Zitto Kabwe Kuburuzwa Mahakamani..IPTL Wadai Alikuwa na Maslahi Binafsi Sakata la Escrow

Zitto Kabwe
Wamiliki wa kampuni ya Independenti Power Tanzania Limited (IPTL) wamefungua kesi mahakamani dhidi ya mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe na mhariri wa gazeti la Raia Mwema.
IPTL wamefungua kesi pamoja na kampuni ya Pan African Power Solutions Tanzania Limited kupinga sakata la Escrow kujadiliwa tena bungeni kufuatia ripoti kadhaa walizozipata, huku wakisisitiza kuwa Zitto Kabwe alikuwa na mgongano wa maslahi wakati alipokuwa akijadili sakata la Escrow Bungeni lakini hakuweka wazi, kinyume cha kanuni za bunge na sheria kwa ujumla.

Katika maelezo yao, IPTL wameeleza kuwa kabla ya kujadiliwa kwa sakata la Escrow Bungeni, walikuwa tayari wamefungua kesi mahakani dhidi ya Zitto Kabwe na mhariri wa gazeti la Raia Mwema, wakiwashitaki kwa kusema na kuchapisha habari kwenye gazeti hilo wakidai kuwa kulikuwa na fedha za umma kwenye akaunti ya Escrow.

Wameeleza kuwa pamoja na kwamba Zitto alifahamu wazi kwamba ni kosa kushiriki kujadili bungeni kitu ambacho una mgongano wa maslahi, lakini aliendelea kushiriki mjadala uliozikandamiza kampuni hizo akiwa kama Mwenyekiti wa kamati ya PAC.

“Mheshimiwa Zitto Kabwe hakuweka wazi uwepo wa kesi hiyo sehemu yoyote katika mjadala wote wa Bunge kuhusu kile kilichoitwa ‘Sakata la Tegeta Escrow’. Kutoweka wazi huko kulipelekea Bunge kupokea taarifa au kupewa taarifa zisizo za kweli kutoka kwa mtu ambaye alikuwa na maslahi katika jambo hilo,” inasomeka sehemu ya pingamizi la IPTL.

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Wanaume wa kigoma mna matatizo gani
    Scandaly zote toka kigoma

    ReplyDelete
  2. Bora ya zitto kuliko domo kulalamika 2 Na ushamba

    ReplyDelete
  3. ASANTENI KWA MATUSI LAKINI KUMBUKENI KIGOMA NDIO YENYEWE HAPO HAMLALI BILA MIZIKI USIKU NA MAJADILIANO,KIBAO . KUMBUKA UBISHI NI ASILI YETU KAMA TUKIONA KITU SIO SAWA ,YEYE ZITTO KISHAKIONA HAPO SOMETHING WRONG LAZIMA ASEME KWA MASLAHI YA UMMA, KWA HIYO HAYA UFISADI BANDARINI WEWE UNA ONA POA TU=`?

    ReplyDelete
  4. Kigoma
    Wasenge, makuchu, mabasha, msago
    Fyuuuuuuuuuuuuuuu

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad