Chadema Watoa Tamko Kuhusu TBC Kusitisha Matangazo ya Bunge Laivu..Kumshitaki Nape Kwa Wananchi

Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrosia na Maendeleo (CHADEMA) Zanzibar, Salum Mwalimu akitoa taarifa yake kwa wanahabari (hawapo pichani).

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimesema kitapeleka hoja kwa wananchi juu ya hatua ya serikali ya kusikitisha matangazo ya Bunge moja kwa moja (live) kwenye Televisheni ya Taifa (TBC) kwa madai kuwa ni kulipunguzia gharama shirika hilo.

Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Zanzibar, Salum Mwalimu amesema kufuatia  kauli ya Waziri wa Habari,Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo iliyotolewa jana bungeni, atapeleka hoja kwa wananchi ili kuona kitendo hicho kama kinakubalika ama la.

Alisema hayo leo katika Makao Makuu ya chama hicho Kinondoni jijini Dar es Salaam, alipokuwa akizungumza na wanahabari, akisema kutorusha matanagzo hayo ‘live’ ni kumnyima mtanzania haki yake ya msingi kwa kuwa matangazo hayo yanalipiwa na  kodi za wananchi wenyewe.

Alisisitiza kuwa haiwezekani kurushwa baadhi ya vipengele, tena nyakati za usiku, muda ambao televisheni nyingi huonyesha vipindi vya burudani na wananchi wengi pia huwa wamechoka kutokana na kazi.

Aliitaka serikali kutaja kiasi cha fedha zinazotakiwa kurusha matangazo hayo ‘Live’ ili atakapopeleka hoja yake kwa wananchi, wakikubali kuchangia, wajue ni kiasi gani kitatakiwa ili hata kama TBC itakataa, wapeleke kwenye televisheni nyingine.

Tags

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hongera CCM wanaficha uozo wao

    ReplyDelete
  2. Kesi yenu haina mshiko mtuletee sisi wananchi eti tuijadili ushuzi mtupu UKIWA fateni yaliyokuwa ya maana kujadili bungeni kuleta maendeleo kwa mwananchi mlalahoi sio kushupalia tuwaoneni live katika tv iweje kuna faida gani tumewachagua mtuwakilishe bungeni ili tuendelee na kazi zingingine sio mtupe kazi ya kukaa kuwangalia kwenye tv na kazi zifanywe na nani ikiwa wote tuko mashughulini na kazi za bunge

    ReplyDelete
  3. Nyie CHADEMA hamna jipya kwa nini hambadiliki siku zote mwatafuta siasa za maji taka kutafuta kiki mtakoma lini malalamiko kila kukicha ili wananchi wawajueni na nyie mpo katika anga za siasa upinzani wa kuishinikiza serikari iwajibike mnatuletee sisi wananchi kazi ipi tuliyo watumeni bungeni ikiwa kila mnaposhindwa kusimamia jambo ktk bunge mnataka kutuletea mazogo mitaani ndio kazi tuliyo watuma bungeni

    ReplyDelete
  4. Kwani pesa za kuendesha hilo shirika zinatokwa kwao au kwetu? simply ni kwetu kupitia kodi zetu. tafadhali lusheni live.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad