Chadema Waungana na ACT -Wazalendo........Wadai Serikali ya Magufuli ni ya kidikteta

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimekosa imani na serikali ya awamu ya tano kwa kuwa na matendo ya kidikteta na kwenda kinyume na katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977 kwa kuminya uhuru wa wananchi wa kupata habari.

Hayo yameelezwa leo Jijini Dar es Salaam, na Kaimu Katibu Mkuu wa Chadema, Salum Mwalimu alipokuwa akizungumza na wandishi wa habari ambapo amesema kuwa serikali imekuwa ikijinadi kwa kauli mbiu ya hapa kazi huku ikiwa mstari wa mbele kwa kuwanyima haki ya msingi wananchi ya kupata habari.

Amesema kuwa matendo hayo ni pamoja na kuzuia Shirikia la Utangazaji la Tanzania(TBC), kurusha matangazo ya moja kwa moja ya mikutano ya bunge inayoendelea ,kufutwa kwa Gazeti la Mawio pasi na sababu za msingi,kuzuia vyama vya siasa kufanya mikutano ya hadhara, na kuunda kamati dhaifu bungeni.

Amesema kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Mnauye ametoa sababu zisizokuwa za msingi ambapo alidai kuwa serikali inaepuka gharama za kurusha matangazo hayo moja kwa moja na baadala yake kurekodi vikao hivyo vya bunge kwa  kurushwa saa nne usiku.

Amesema inaonekana Waziri huyo hajafanya utafiti na kwamba ikiwa  tatizo lipo kwenye gharama alizotaja chadema ipo tayari kuchangia gharama hizo kwa kuanzisha harambee maalumu pamoja kuwataka chama cha wamiliki wa vyombo vya Habari (Moat) na Baraza la Vyombo vya Habari (MCT) kulisimamia suala hilo.

“Nape ataje gharama hizo tutachangishana ......mwenye mia moja mia mbili ili wananchi wajue mambo muhimu yanayoendela kwa wakilishi wake”,amesema Mwalimu.

Amesema Nape alikuwa anayumba kwa kuwa na ndimi mbili kwa kuongeza sababu nyingine ya kuzuia kurusha kwa matangazo hayo ni kuwa muda huo ni wa kazi na kwamba watu watakuwa hawafanyi kazi kutokana na kuangalia bunge.

Amesema kuwa hoja ya watu kutofanya kazi haina mashiko kutokana na watu huwa wanafanya kazi ilhali bunge linaendelea ambapo kama kuna hoja muhimu watu huzisikia bila kuathiri shuguli zao lakini kuna wengine muda huo sio wa kazi kwao.

Amesema kuwa serikali imekusudia kuminya uhuru wa habari kutokana na matukio yaliyofuatana ya kushugulikia vyombo vya habari.

Amesema kuwa serikali imezuia mikutano ya siasa ambapo Waziri Mkuu Kasimu Majaliwa na Nape Mnauye walitoa kauli hizo walipokuwa Mkoani Lindi na baadaye Jeshi la Polisi kuweka mkazo wa suala hilo.

Amesema suala hilo hawawezi kulikubali kutokana na chama kuwa na mikutano yao kila baada ya muda na kwamba muda wa kuratibu mikutano hiyo watafanya vikao vyao.

Amesema serikali imeunda kamati dhaifu bungeni  kwa nia ya kudhoofisha shughuli za utendaji bungeni na maendeleo ya nchi kwa kuwaweka wabunge wageni kwenye kamati muhimu ilhali hawana uwezo kuzisimamia ambapo kamati ambazo hazina umuhimu kupangiwa watu wenye uwezo.
Tags

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. kazeni buti, msitetereke tunawategemea.

    ReplyDelete
  2. SI WAPINZANI,SI WA CCM,KWA UJUMLA TANZANIA YA SASA INAELEKEA KUKOSA ADABU,HAIVUTII TENA KAMA ENZI ZA NYERERE & KARUME.
    MUNGU WETU TUNAKUOMBA UTUONYESHE NJIA INAYOPASWA KUFUATWA.

    ReplyDelete
  3. Rais Wangu Eng. Pombe Joseph Magufuli kaza buti tuletee Maendeleo...tunaunga mkono jitihada zako za kubana matumizi....keep it up

    ReplyDelete
  4. Ninyi CHADEMA acheni hizoo! Mbona hamuongelei mafisadi na wauza unga wanaokamatwa na mali zao kutaifishwa? Mnag'ng'ania swala la TBC kupunguziwa muda wa kuonesha vikao vya Bunge, lina tija gani swaala hilo? Tena ningependa wazuie kabisa kwani ninyi wapinzani mmetumia vibaya fursa hiyo. Mnatoa hoja za ushabiki na ugangwe hata pale ambapo hamstahili kupinga. Hatutaki hoja za show. Ongeleeni huko huko gizani, tutawapata kwenye hansard.

    Mgeshika ninyi Dola, walahi umaskini ungetuua. Nchi hii ingekuwa ya wachache na ingeuzwa kwa makabulu. Chadema hamfai kabsaaaaaa!

    Hapa Kazi Tu haina mbadala.

    ReplyDelete
  5. hahahaha ona sasa mbowe alivyo muhuni anajipendekeza ACT makusudi ili awahadae kwenye ukawa
    yani chadema ndio madikteta apa Tanzania manake
    ukabila wao mafisadi wao sera mbovu wao kazi kususia vikao vya bunge mbona na posho hamsusi
    mikundu kunuka nyie ukawa

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad