Dawasco Yaibua Wizi Mwingine wa Maji Unaofanyika Katika Kiwanda cha Maji ya Betri


Moja ya kisima kinachodaiwa kutumika kuhifadhi maji yanayodaiwa kuibwa kutoka katika mtandao wa maji wa Dawasco.

Madumu ya Maji ambayo yame3kuwa yakitumika katka utengezaji wa maji ya Betri katika kiwanda cha Bahari Chemicals Ltd .

Sehemu ya wizi wa maji kutoka katika mtandao wa DAWASCO unavyoone3kana kufanywa katika kiwanda cha kutengenezea Betri cha Bahari Chemicals Ltd.

Ikiwa siku chache tu zimepita baada ya shirika la Majisafi na Majitaka Dar es salaam (Dawasco) kubaini wizi mkubwa wa Maji kutumika katika shamba la mboga mboga na matunda katika chuo cha Islamic kilichopo Boko ununio jijini Dar es salaam. Dawasco imebaini wizi mwingine wa Maji katika kiwanda cha kutengeneza Maji ya betri cha Bahari Chemicals Ltd kilichopo kurasini wilaya ya Temeke jijini Dar es salaam.
Akizungumzia tukio hilo meneja wa Dawasco Temeke, Bw. Deogratius Rwegasira, amethibitisha kutokea kwa wizi huo ambapo kiwanda hicho kilikuwa kimejiunganishia Maji bila kibali cha Dawasco na kwamba hawakuwa na mita wala akaunti namba inayoonyesha kiasi cha Maji kinachopita katika system ya Maji iliyopo, na baada ya kufanya mawasiliano na Mkurugenzi wa kiwanda hicho Bw.Devendra Singh Parmar amekiri kutumia Maji hayo kinyume na taratibu .
“Baada ya kufanya uchunguzi tumebaini kuwa kiwanda hiki kimekuwa kikituibia Maji yetu kwa muda mrefu, mmiliki wa kiwanda amekubali kosa,lakini akisema kwamba wenyewe ni wageni hapa hawana zaidi ya mwaka mmoja tangu waanze kazi.hivyo hawakujua taratibu za kufuata”. Alisema Bw. Rwegasira.
Aidha meneja wa kiwanda hicho, Bw. Abdul Gulam, amekiri kuihujumu Dawasco kwa kuiibia Maji, lakini amesema kuwa wao ni wapangaji tu wamepanga katika eneo hilo na wana muda wa miezi saba tangu wahamie kiwandani hapo, walikuta wizi huo wa Maji ukifanyika katika kiwanda hicho na hawakujua taratibu husika za kufuata ili wapate huduma ya Maji kihalali.
“Sisi tumekubali kuwa tulikuwa tunatumia Maji ya DAWASCO bila kuyalipia, lakini sio sisi ambao tuliounganisha bomba hili, wapangaji waliopita walijiunganishia Maji haya hivyo tunaomba tulimalize hili, ili tuanze kuwa wateja wenu rasmi” alisema Bw.Gulam.
Aidha bwn Gulam ameainisha kuwa wao kama wamiliki wa kiwanda wamekubali kulipa faini iliyotolewa na DAWASCO ya Shiling million 3.5 ili warudishiwe huduma kama wateja wengine na waweze kuendelea na biashara.
Vitendo vya uhujumu wa Miundombinu ya Maji hususani wizi wa Maji unaendelea kuwa changamoto kwa DAWASCO licha ya kampeni na elimu inayotolewa kila siku juu ya uhalali na utaratibu wa kuungiwa huduma ya Maji inayotolewa na DAWASCO.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad