Diamond Platnumz amechukizwa na jinsi wasanii anaowaheshimu wanavyohaingaika kumchafua yeye na mwanae Tiffah mtandaoni na amesema tayari anawajua wasanii hao.
Akizungumza kwa hasia na Ayo TV Alhamisi hii, Diamond alisema anawashangaa wasanii wanaotumia muda mwingi kumponda mtoto wake kuliko kutafuta pesa.
“Watu wamekaa kwenye sanaa muda mrefu mimi nimewakuta, nawaona wameanza kuwa mastaa kabla ya mimi, hawana viwanja, hawana nyumba, hawana magari. Wangetumia muda huo kutengeneza maisha yao kuliko kukaa kumdis mtu mwingine. Halafu mimi sipendagi kusema lakini inavyofika hatua kwenye vitu kama hivi mimi naongea. Kwanza nilikuwa sijui uchungu wa mtoto sasa hivi naujua kwamba kweli mtoto anauma,” alisema Diamond.
“Halafu mtu anayezungumzia inawezekana mtoto akawa na pesa kuliko hata yeye, kwa sababu akaunti ya Tiffah inawezekana ikawa na hela hata kuliko huyo mtu anayemdiss huyo mtoto kama sio wangu mimi. Inawezekana akawa na hela kuliko hata wewe unayesema mtoto sio wangu au unasema mtoto mbaya. Kwa sababu mtoto alifunguliwa akaunti yake kwa mara ya kwanza ikaingia milioni 10. Ni mtoto inawezekana ni maarufu kuliko hata wewe kwa sababu nikifika Nigeria wanaanza kuuliza Tiffah hajambo? So inafikia time hata kwa mtoto unataka kiki?”
“Kwa ndugu zangu wasanii waache kidogo kumfuata fuata binti yangu, kila mtu anakuja sijui DNA sijui nini, waache hizi mambo mimi ndiye mwenye mtoto.”
Tazama mahojiano hayo hapo chini
Download Android Application ya Udaku Special Blog Kupata Udaku Kirahisi Kwenye Simu yako ..Bonyeza HAPA Kudownload Kutoka Play Store
Waswahili sana hawa wadanganyika mondi bin laden kazi kushupalia maisha ya watu kwenye social media na team zao ushuzi,you all motherfucker mind your bizness leaves baby alone,uswahili kazi sana too much drama wasahili tafuteni kazi za kuingiza vipato
ReplyDeleteyeye mwenyewe mswahili tena wa tandale nakukumbusha tu
DeleteNakupenda usivyojali,sasa mwambie na mama T aachane na majibizano ya kijinga,akae kimya ndio itanoga zaidi.Tiffa awe wako au sio wako kipi kinawagharimu?manina zao.
ReplyDeleteACHANA NAO BRO!KAA KIMYA KUANZIA LEO.
ReplyDeleteDIAMOND KAZA BUTI ACHANA NAO HAO. PIGA KAZI WEWE ACHA WASEME USIKU WATALALA. BRAVO BABA TIFFA. HUYO ANAYEULIZA DNA YA TIFFA MUULIZE YEYE ANA HAKIKA HUYO ANAYEMWITA BABA NI BABAKE KWELI??????????????????????????????????
ReplyDeleteNimependa speech yako Dai. Watanyooka tu. Dai oyeeee
ReplyDeletewewe unayetaka DNA ya tiffa hebu kapime na wewe utuambie huyo unamwita baba kama ni BABA yako kweli!!
ReplyDeleteikumbukwe diamond kaleta mapinduzi makubwa sana katika mziki wa bongo, bei za shoo yeye ndo kabadilisha kulabo za njee na hata kuwa nominated BET awards
ReplyDeletehao wasani wakubwa waliotangulia wameshindwa kufanya chochote katika mziki wa bongo wameishia kukimbilia siasa wakijua siasa dili tena kwa maslai yao
diamond hata mumseme vipi level zake ni za kimataifa na mziki wake unakuwa kila siku
ttz wasani wengi wa bongo hawana elimu ya sanaa na hawapendi kazi zao fanya yako diamond umewafungua macho lakn bado hawaoni shauri zao waendelee kudiss hao wanamitoto kibao wameitelekeza kwa mama zao
Msichanganye mada hapa, hakuna aliyemwambia mziki wake mbaya. Hata huko kujilikana kimataifa ni kwa faida yake mtanzania wa kawaida anafaidika nini na mziki wake?
DeleteWao wanadiss sana wenzao wakijibiwa wanakimbilia kwenye interview what for? Kunya anye kuku akinya bata kaharisha - aaah wapiii
Ama kweli mtenda akitendewa hujihisi kaonewa. Mmelikoroga wenyewe lazima mlinywe
hasira za mkizi hizoo. yeye akiwatukana wasanii wakae kimaya akijibiwa inakuwa issue. aache uswazi
ReplyDeleteNDO WAMJIBU KWA KUMSEMA TIFFA???MTOTO HATA HAJUI KITU MWACHENI JAMANI.
ReplyDeleteNawe ktk watu wenye pesa unajiweka
ReplyDeleteShule bwana kazi siku hizi naye ukiongea unachanga Na kizungu Fyuuuu
Tongo tongo za macho tukutoe sisi leo una domo
Nani anashida Na wewe
Tena hao wanakuja kuangalia muziki ni washamba boycott huyu
Diamond binadamu hawana jema, hapo hata ukipima hiyo DNA na ikionesha tiffah Ni damu yako bado watakusakama watasema umefoji majibu sababu hayajatoa majibu Yao. Chamsingi Ni kuwapotezea, hao wanaotaka DNA wenyewe hawajui hata mimba zao wamepewa na nani. WAnaacha kuhangaika na dna zao kwanza wanapiga kelele na ya malaika tiffah. Akili mgando hizo, fanya yako achana nao dogo.
ReplyDeleteMNAMWONEA WIVU DAIMOND JAMANI MWACHENI MUNGU KAMJALIA
ReplyDeleteWatanzania acheni vurugu zisizokuwa na maana, Diamond ni mswahili saaaana yeye kama yeye asingewajibu lakini hawezi kujizuia hata kidogo sidhani kama alipata malezi mema ni bahati tu kwamba Ana kipaji cha kuimba lakini tabia yake ya uswahili ipo wala haijifichi jamani na mnaosema asipime DNA ni Wale Wale mnasahau Kuwa yeye ni kioo cha jamii , angekaa kimya sidhani kama watu wangehitaji kujua zaidi lakini mashauzi yamezidi nawajua watu wa ujiji kigoma Ndio zao ni waswahili kupindukia asili haachi asili. Sidhani Mimi Kuwa watu wanamuonea wivu ni kwa sababu ya mdomo wake aache masauzi ya kike aone nani atamfuatilia NO BODY!!!
ReplyDeleteKwakwaaa lol! Jamani mambo si mwanzo mwishoo cheeei! Alianza na ultra sound sasa DNA kisha mambo yasogee n mbeleee Hihiii tunyooke tuu
ReplyDeleteKILA ZAMA NA KITABU CHAKE! VITABU VYENU VIMEPITWA NA WAKATI ACHENI KITABU CHA NASEEB KING'AE! HUO NDIO UKWELI HAKUNA UBISHI HAPO! HUYO YUKO JUU TUU HATA MUMSEME VIPI!
ReplyDelete