Akizungumza na mamia ya watu waliojitokeza kumpokea katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (Kia) na barabara kuu ya Arusha -Moshi, Dk Magufuli alishukuru kwa mapokezi aliyopata na kusema hatawaangusha wananchi hao.
“Uchaguzi umekwisha ndugu zangu sasa ni kazi tu na wananchi wa Arusha na Kilimanjaro sitawaangusha, ahadi zangu zote nilizotoa wakati wa kampeni nitazitekeleza,” alisema.
Alisema anajua matatizo ya Arusha na Kilimanjaro na kama alivyoahidi atatekeleza yote.
Pia Mh John Magufuli amesema kuanzaia sasa hataki kusikia malalamiko ya wananchi juu ya suala la njaa na ikitokea akasikia vilio hivyo vikiendelea mkuu wa mkoa husika atachukuliwa hatua ikiwemo ya kufukuzwa kazi.
Mh. Magufuli ambaye yuko katika ziara ya kikazi mkoani Arusha ameyasema hayo alipokuwa njiani kutoka jijini Arusha kwenda wilaya Monduli kwa ajili ya kufunga mazoezi ya kijeshi ya kuonyesha uwezo wa medani 2016 yaliyofanyika katika Briged ya 303 iliyoko Monduli
Dah,yaani mie sikujua kama huyu baba akiwa rais atapendwa na watanzania wengi hivi,Nisamehe Mungu wangu kwa kumnyima kura huyu JPJM.
ReplyDeleteWera baba,wera!
ReplyDeleteKikwete kawaweza ama kweli wameula wa chuya waliomtabiria CCM itamfia kusema ukweli kalamba turufu angezubaa CCM ingekuwa hisitoria
ReplyDeletehadi arusha wamemkubali
ReplyDeleteukabila tupa kule apa kazi tuu