Dkt. Kigwangala Amtembelea na Kumjulia hali Mwadhama Kardinali Pengo.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dkt. Hamis Kigwangala jana alimtembelea na kumjulia hali Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mwadhama Kadinali Polycarp Pengo aliyelazwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete iliyopo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam.

Akiongelea kuhusu hali ya Kadinali Pengo, Mhe. Kigwangala alisema kuwa Kadinali Pengo yuko salama katika mikono ya madaktari wa taasisi hiyo na hali yake inaendelea vizuri ambapo ameweza kuongea nae ana kwa ana kiasi cha kuweza kukaa na kuongea.

‘’Mwanzoni alilazwa katika Hospitali ya TMJ iliyopo hapa jijini Dar es Salaam, lakini ikaonekana ni vema akiletwa hapa kwenye Hospitali yetu hii ya juu kabisa ya matibabu ya moyo (Tasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete), hivyo napenda kuwapa taarifa Watanzania kwamba yuko salama kabisa katika mikono ya madaktari wetu na hali yake inaendelea vizuri.’’

Awali Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Magufuli akiongozana na Mkewe mama Janeth Magufuli walienda pia kumjulia hali Kadinali Pengo katika taasisi hiyo na kumtakia afya njema ili aweze kuendelea na shughuli zake za kiroho.

Kadinali Pengo alifikishwa katika taasisi hiyo ya moyo kwa ajili ya kuchunguzwa afya yake ambapo afya yake kwa sasa imezidi kuimarika.

Hapa  kuna  video  nzima ya Dr. Kigwangala  akimjulia hali

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad