Edward Lowassa Alalamikia Wafuasi wake Kuandamwa na Watendaji wa Serikali.

Aliyekua mgombea Urais wa Chadema anayeungwa mkono na vyama vinavyounda UKAWA Mh.Edward Lowassa amelalamikia baadhi ya watendaji wa serikali kwa kuwaandama na kuwatisha wananchi na wafanyabiashara waliokuwa wanaunga mkono vyama vya upinzani na amezitaka idara zinazohusika kuchukua hatua ili kuepusha  matatizo yasiyo ya lazima.

 

Akizungumza katika ibada maalum ya kukaribisha mwaka mpya iliyofanyika katika kanisa la kilutheri wilayani Monduli Mh Lowassa amesema amepokea malalamiko ya kuwepo kwa uonevu  na vitisho kwa wadau walioonekana kuunga mkono vyama vya upinzani licha ya kuwa ni haki yao kikatiba.

Pia Mh Lowassa aliyekuwa mbunge wa jimbo la Monduli kwa tiketi ya  (CCM) kabla ya kuhamia Chadema na kuwa mgombea urais amesema ataendelea kusaidiana na mbunge wa sasa Mh Julias Kalanga (Chadema) kutatua kero za wananchi na kuhakikisha kuwa misingi aliyoijenga inakuwa endelevu.

Kwa upande wao baadhi ya viongozi wa dini na wananchi waliohudhuria ibada hiyo wamepongeza uvumilivu wa kisiasa ulioonyeshwa na Mh Lowassa ambao umeendelea kuimarisha amani na utulivu  nchini na wamewaomba wanasiasa wengine kuiga mfano huo.

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Tutoleeni s iasa taka. Rais tuliyenae anatutosha Mungu mlinde Rais wetu mpendwa JPJMAGUFULI.

    ReplyDelete
  2. hiyo pete imekupendeza mzee

    ReplyDelete
    Replies
    1. Pete za kikwete mikono yote
      Mbona hausemi

      Delete
  3. Wewe mwenyewe Fasidi mkubwa ni bora nenda kachunge

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad