Washindi wa tuzo za Oscar, George Clooney na Mkenya, Lupita Nyong’o pamoja na muigizaji wa Uingereza David Oyelowo wameungana na mastaa wengine waliopaza sauti kutaka kuwepo mabadiliko kwenye tasnia ya filamu na akademi ya sanaa ya picha zitembeazo na sayansi ambayo wajumbe wake walitaja majina ya waigizaji weupe tu kwenye tuzo za Oscars 2016 kwa mwaka wa pili mfululizo.
Clooney alisema kuwa Academy ilikuwa ikifanya vizuri zaidi miaka 10 iliyopita ambapo waigizaji weusi walikuwa wakipata nafasi.
Muongozaji wa filamu Spike Lee, anayeongoza wito wa kuzisusia tuzo hizo ametaka kuwepo kwa hatua stahiki ili kuleta usawa katika matabaka mbalimbali kwenye Hollywood.
Lee, aliyewahi kupewa tuzo ya heshima ya Oscar, amedai kuwa Hollywood ipo nyuma ya muziki na michezo katika kutambua watu wa matabaka mengine tofauti na weupe.
Mwingine aliyepo mstari wa mbele ni Jada Pinkett-Smith, mke wa Will Smith aliyeigiza filamu ya Concussion ambayo haijatajwa kwenye tuzo hizo. Jada amedai kuwa pamoja na watu weusi kutumika kukabidhi tuzo na kuburidisha, tuzo hizo zimeshindwa kutambua mchango wanaoufanya kwenye filamu zao.
Naye Lupita ametumia Instagram kupost ujumbe huu:
Pinkett na Lee wamesema hawatahudhuria tuzo hizo zitakazotolewa February 28. Asilimia 94 ya wajumbe wa academy hiyo yenye watu zaidi ya 6,000 ni weupe na asilimia 77 ni wanaume.
Hivi karibuni Academy imeanza kuongeza wajumbe wapya wakiwemo host wa tuzo hizi mwaka huu, Chris Rock, Lupita Nyong’o, muongozaji wa filamu ya Selma, Ava DuVernay, mchekeshaji Kevin Hart na Steve McQueen, muongozaji wa filamu ya , 12 Years a Slave.
Kwa sababu waafrica tuna nyodo sana Na vishindo
ReplyDeleteSi tuanzishe ya kwetu Africa basi uonne watakaopewa
Tuna matatizo nenda Haiti si Africa lakini Kama Upo kariakooo
Kisa rangi yetu
Nenda South Africa wanakoishi wazungu Kama Upo ulaya Au USA
Tujiulize kulikoni
hili neno
ReplyDeleteHata BET si inakuwa na weusi tu. Wasiende tu kwenye Oscars wasubirie BET Awards watapewa zao.
ReplyDeletewaafrica ngozi ya pumbu
ReplyDeleteanagalia ulaya matororisti wote na wabakaji toka north africa
fyuuuuuuuuuu
osaca ni kwa weupe au waafirca wenye asili ya ulaya na usa
Kwa Africa ni viongozi wetu wenye inferiority complex kwa wazungu. Hawajiamini, hawana fikra chanya, wanauza maligafi au kutoa bure kwa Wazungu na kuwaacha Waafrika wenye elimu, chapa kazi na Wazalendo. Wanawanyanyasa Waafrika wenzao nchini na kujiweka karibu na Wazungu bila haya. Ni hawa viongozi wetu wasio na majivuno, wanatumika kuwa vijibwana wa Wakoloni sababu wanawanyima maendeleo Waafrika sababu za wivu na kutokuwa na ustaarabu.Wanawanyenyekea Wazungu hata wale ambao hawanazo juu. Hii inasababisha Wazungu kuwadharau Waafrika wote. Lakini Waafrica mngechagua viondozi Wazalendo, mkaweka sheria na kuzifuata, hatungedharauliwa Duniani. Wazungu wanafaidika sana Africa nzima sababu mmewaruhusu wawatawale kuanzia mabenki mnayoyaruhusu na wanapata faida mabilioni na kupeleka kwao. Madini MMewapa maraisi wa nje, bila hata malipo. Uranium, mnawapa bure wanatengeneza mabomu kuja kuwauzia muuane,Meno ya tembo ni mtaji mkuu wa Wachina na wengi walio Africa hata kisomo hawana.Mnaletewa makopo yasiyo na thamani toka china na yanaua viwanda bora Africa. MMewapa Ardhi za Wananchi na kuwatengea maeneo mazuri na mwafrika kukanyaga mwiko, unatumiwa mbwa. Mnaletewa silaha muuane nyinyi kwa nyinyi na kuzoofesha jamii. Je ni nani anaruhusu haya? Sheria kandamizi, Wivu, ufisadi, , kutokulipa kodi, unamwnua mtu mweupe mwenyewe kokote duniani na nchini kwako na anakugombanisha wewe na jirani. Nyinyi maraisi na viongozi wa nchi je hamjayafanya haya? Mbonamagufuli kayaona na mnamwekea mizengwe. Mungu ibariki Africa, Badili mfumo wa kufikiri, lete amani msaidie Mwafrica aamke na kujikomboa mwenyewe kielimu, kiutendaji, na rudisheni dini zenu na muwaheshimu wahenga wenu. Mmewadharalisha mno.
ReplyDelete