Hali si Shwari Bandarini..Si Wizi Bali Kufuru..Meli Nzima Yaibwa, Wanjanja Waficha Nyaraka Kuonyesha Haikuwahi Kufika Tanzania

Makubwa yamezidi kugundulika kwenye sakata la upotevu wa makontena Bandari ya Dar na sasa inadaiwa kuwa kuna nyakati wahusika wamewahi kufuta kumbukumbu za meli nzima ya makontena na kuiba makontena yote.

Taarifa hizo zinavuja wakati kukiwa na mvutano kati ya chama cha Mawakala wa Forodha Tanzania (TAFFA) kinachodai kutohusika kwa namna yoyote na upotevu wa makontena zaidi ya 11,000 ambayo hayakulipiwa ushuru bandarini (Wharfage charges).

TAFFA wanaitaka Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), kuwajibika katika upotevu huo ulioinyima Serikali kupitia mamlaka hiyo mabilioni ya fedha.

Chanzo: Raia Tanzania

Udaku Special Blog
Tags

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Uwiiiiiiiiiiiii,hivi kuna sababu kweli Tanzania kuitwa nchi maskini na kutegemea kuombaomba misaada?Mungu wetu endelea kututetea wanyonge,Ibariki serikali ya Tanzania chini ya JPJM.

    ReplyDelete
  2. hivi hao viongozi wa awamu iliyopita, walikuwa wanafanya nini jamani? dah!! meli nzima inaibiwa? hatari hii!!!

    ReplyDelete
  3. Hayo ni tuliyoyasikia mpaka sasa. Tafakari tusiyoyajua! Ndio maana waatu walizidi ujeuri, na ninaelewa kwa nini wadada wengi walipigania Fisiem wabaki madarakani.

    ReplyDelete
  4. Yaani ni pure kichefuchefu kuzisoma habari kama hizo wakati wote mnaujua mwisho wake kuwa hakuna mtu/watu atakae/watakao tajwa kuwa ndio muhusika/wahusika ili sheria ichukue mkondo wake hiyo ndio bongo kuna WAKOLONI "WEUSI WACHACHE" wanaowatala weusi wenzao walio wengi kimabavu in the name of democracy

    ReplyDelete
  5. Jipu hilo sasa kitambo litatumbuliwa na kama ni kansa basi sehemu ya mwili ni kukata kabisa ili mhusika abaki nusu

    ReplyDelete
  6. Tena watuambie ya Lowassa ni mangapi, maana ni yeye tu ndio alikuwa anasemwa kwa ufisadi. Hahaaaa Mkwereeee.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad