Aliyekuwa mgombea urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa, amemtembelea Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye, katika taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Hosptitali ya Taifa Muhimbili alikolazwa.
Lowassa ambaye alifika hospitalini hapo jana saa 7:00 mchana akiwa na mke wake Regina, aliwapongeza viongozi wengine ambao wamekwisha kufika hospitalini hapo kumjulia hali Sumaye, wakiwamo Rais John Magufuli, Rais Mstaafu na Mwenyekiti wa CCM, Jakaya Kikwete na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.
Lowassa alisema hilo ni jambo jema la kiungwana, la kuheshimiana na kutendeana mema.
Wengine waliomtembelea Sumaye hospitalini hapo ni Waziri Mkuu Mstaafu, Dk. Salim Ahmed Salim na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Prof. Mwesiga Baregu.
Nyie udaku poa kabisa simlituonyesha picha kuwa afya ya Edo imetengemaa yupo Chadema mbona twamuona hapo akimsalimia Sumaye yuko vilevile kachoka
ReplyDeleteSafi sana umefanya vyema kwenda kumjulia hali kamanda mwenzio wa mabadiliko. Peoples Powerrrrr
ReplyDeleteSafi sana umefanya vyema kwenda kumjulia hali kamanda mwenzio wa mabadiliko. Peoples Powerrrrr
ReplyDeletelowassa nampenda sana kila nikimuona picha zake chozi linanitoka
ReplyDeletekiukweli LOWASSA ana busara na hekima iliyojitosheleza
ReplyDelete