Hivi Escrow ni Ufisadi au Promotion? Wahusika Bado Wanapeta na Kukabidhiwa Vyeo....

Tumeshuhudia watuhumiwa wa Escrow wakikabidhiwa Wizara na Idara Muhimu za Umma na wengine kupitishwa kugombea Ubunge wa kwenye Serikali ya awamu wa Tano kana kwamba hawakufanya Ufisadi wa aina yoyote, kwenye Serikali ya awamu wa nne. Pengine mimi naweza kuwa sina Ufahamu wa kutosha juu ya maana ya neno Ufisadi.

Hebu tujiulize, unawezaje kufumbia macho Ufisadi wa Escrow zaidi ya bilioni 300, na wakati huo huo ukasema unatumbua jipu kwa ufisadi bilioni 59? Namaanisha bilioni 12 za makontena TRA na 47 za makontena bandarini. Na usimpeleke mtu hata mmoja mahakamani, na wakati huo huo ukamkabidhi uongozi, Wizara na Idara muhimu za Umma.

Kwa uelewa wangu hapa kuna double standard na maana halisi ya Kutumbua jipu inageuka kuwa uonevu na kuoneana haya.

Je, ni lini watuhumiwa hawa wa Escrow walifikishwa mahakamani kujibu tuhuma za Ufisadi wa Escrow na Mahakama ikawasafisha, na wakastahili Promotion hii?

Prof. Muhongo - Waziri Nishati na Madini

Maswi - Ag D. Commissioner TRA.

Chenge - Mbunge.

Tibaijuka - Mbunge.

Ngeleja - Mbunge.


Je, Escrow ni Ufisadi au Promotion?

" Injustice anywhere is a threat to justice everywhere" M.L. King Junior.
Tags

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Tanzania ina wenyewe

    ReplyDelete
  2. acha siasa za majungu tafuta kazi ya kufanya kulikomboa taifa na si story mfano wakati unajiuliza escrow ungeenda kumuuliza diwani wako anamipango gani ya maendeleo

    ReplyDelete
  3. Hivi watanzania wengine wana shida ya kufikiri? Chuki ya mtu na mtu aina nafasi kwa sasa. Sasa hivi ni kazi tuu. Majungu serikali ya a wa mu ya tano no.

    ReplyDelete
  4. wote tunashangaa kwa nini fisadi aliyesumbuliwa sana ni lowassa na wengine ni mafisadi wapendwa na wasifiwa.??????

    ReplyDelete
  5. Na bado Makonda mkuu wa mkoa nyeti
    Hapa kazi tu ccm hiyo

    ReplyDelete
  6. Majizi Piga yote mittani Choma moto kama vibaka Kama ccm haiwaadhibu

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad