JE Unahabari Kuwa Yule Chinja Chinja wa Wanamgambo wa Kundi la Islamic State Aliwahi Kuja Tanzania!

Jihadi John, mwanamgambo wa kundi la Kiislamu la Islamic State ambaye amekuwa akisakwa sana na maafisa wa Marekani na Uingereza amewahi kutua Tanzania.

Hata hivyo, mwanamgambo huyo ambaye jina lake la kuzaliwa ni Mohammed Emwazi, hakuruhusiwa kuingia baada ya kuchunguzwa uwanja wa ndege na alipandishwa ndege na kurejeshwa Ulaya kupitia Uholanzi.

Hii ilikuwa ni Agosti 2009, wakati huo akijiita Muhammad ibn Muazzam.
Emwazi alifika Tanzania akiwa ameandamana na Mwingereza mwingine kwa jina "Abu Talib" na Mjerumani anayejulikana kama "Omar".

Watatu huo waliwasili uwanja wa ndege Dar es Salaam wakidai lengo lao lilikuwa kutalii nchi, baada ya kumaliza masomo ya chuo kikuu.

Hata hivyo, walizuiwa kuingia na baadaye Emwazi aliambia shirika la kutetea haki la Cage jijini London kwamba walidhalilishwa na kuteswa.

Lakini afisa mmoja wa polisi nchini Tanzania ameambia BBC kwamba Emwazi alifurushwa kwa kuwa mlevi na kwa utovu wa nidhamu.

Afisa huyo alisema Emwazi “alileta vurugu uwanja wa ndege” kwa kuwa “mwenye fujo na kelele nyingi” na kwamba alionekana kama alikuwa amelewa.
Hayo yalimfanya yeye na wenzake kuzuiwa kuingia.

Emwazi baadaye alidai kwamba alitishwa akiwa ameelekezewa bunduki na kwamba aliambiwa aulize serikali ya Uingereza sababu yake kuzuiwa kuingia.

Lakini kamishna wa uhamiaji wa Tanzania Abdullah Khamis Abdullah alisema hakuna maagizo yoyote yaliyokuwa yametolewa na taifa la nje kumzuia Emwazi kuingia.
Afisa aliyemzuiliwa Emwazi pia alisema hakuteswa kama alivyodai.

Shirika la Cage lilisema Emwazi alihojiwa na maafisa wa usalama wa Uholanzi na Uingereza aliporejea nyumbani kupitia Uholanzi.

Habari alizotoa ni pamoja na madai kwamba idara ya ujasusi ya MI5 iliwasiliana na mchumba wake, na hilo likafikisha kikomo uhusiano wao. Emwazi mwenyewe hakushtakiwa kwa makosa yoyote.
Idara ya MI5 inaamini safari hiyo ya Emwazi haikuwa safari ya kawaida kama alivyokuwa akidai.
Alikuwa amehusishwa na washukiwa wakuu wa kijihadi ambao walikuwa wakifuatiliwa na idara hiyo pande mbalimbali duniani.
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Asante Yesu kwa ulinzi na upendo kwa nchi yetu..

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad