Jee Mnatambua Kuwa Baadhi ya Maamuzi ya Magufuli, Yanaligharimu Taifa Kiuchumi?

Kuna watu wanashangilia sana kila kinachofanywa na Magufuli, wakidhani ndio the right thing!. Mfano alipoamua kuunda baraza dogo la mawaziri, na kuongeza idadi ya makatibu wakuu, badala ya kupunguza gharama, kutaongeza ghara za uendeshaji!, serikali ni makaribu wakuu ambao ndio waendeshaji, na sio mawaziri!.

Mfano wanaposikia maofisa wakuu fulani wa umma, wamesimamishwa kazi, na kuteuliwa wengine kukaimu nafasi zao!. Hatua hii kisiasa ni nzuri, maana ina mpa kick Magufuli kwa boost political mileage yake, ila kiuchumi, Magufuli analibebesha taifa hili mzigo kubwa kuliko hata serikali ya JK!.

Kwa mujibu wa sheria za kazi, kila mtumishi aliyesimamishwa kazi kwa tuhuma zozote, anaendelea kulipwa mshahara wake kamili, bali maupurupu ndio yanaondolewa!.

Mtumishi atalipwa nusu ya mshahara iwapo atasimamishwa kazi na kushitakiwa, na mtumishi hatalipwa lipwa mshahara iwapo atafukuzwa kazi!.

Tangu Magufuli aanze hii timua tumua, hakuna ofisa mkuu yoyote aliyefukuzwa, wala aliyeshitakiwa, wate wamesimamishwa tuu kusubiri kupangiwa kazi nyingine!, wote wanaendelea kulipwa mishahara yao ile ile!.

Hata upande wa uteuzi wa Makatibu Wakuu, wale makatibu wakuu wote ambao ukatibu wao mkuu haukutenguliwa, wanaendelea kulipwa mishahara ya makatibu wakuu kusubiri kupangiwa kazi nyingine!.

Hivyo baadhi ya hatua zinazochukuliwa na rrais wetu John Pombe Magufuli, japo ni hatua nzuri, na zimefanywa kwa nia njema, zitaligharimu sana taifa hili!, ni bora Magufuli angefuata ule mtindo wa Nyerere, ilikuwa hakuna kusimamisha kazi, ilikuwa ni kufukuza tuu!. Anapounda baraza jipya na kutea makatibu wakuu wapya, wale wote walioachwa, walikuwa wanastaafishwa kwa manifaa ya umma na mishahara yao inasimamishwa kuanzia hapo!.
Happy New Year

By Pasco-JF

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hivyo mshara wa waziri na katibu mkuu unalingana hata robo yake? Wakati wa kufukuzwa kazi katibu mkuu kwa kosa la waziri hauna nafasi katika serikali ya maghuful mtu atahukumiwa kwa kosa alilotenda hahihalisi awe waziri au mkurugenzi hapa kazi tu. System ya kuajiri makatibu wakuu wakutosha kwa kila wizara ni nzuri sana na ni ya kupongezwa mno kwa magufuli(he is so genius) kwa sababu baada ya kurundika rundo la mawaziri maofisini muheshimiwa raisi ameamua kujaza watendaji kwa ajili ya kuharakisha ufanisi zaidi. Alichokifanya muheshimiwa Magufuli ni mfano wa kuajiri wapishi wachache mahiri na kuwapatia wahudumu wa kutosha wa kuwasambazia huduma kwa wateja kwa haraka zaidi si dhani kama hapo kutakuwa na malalamiko kutoka kwa wateja. Na kusema kwamba hao watumishi wazembe waliosimamishwa kazi kudai kwamba wanasubiri kuhamishiwa sehemu nyengine za kazi labda hapo humzungumzii magufuli kama raisi wa nchi hii hivi sasa. Ni pumba zisizo na mshiko wa aina yeyote. Kwa kwanza maghufuli hata kazi hajaanza hayo aliyoyaanza kuyafanya ni kama salamu tu kwa watumishi wa umma. Hao wezi au wazembe waliokuwa wakilitia hasara taifa hili ni bora wakae nje wakilipwa maisha mishahara ya halali bila ya kufanya kazi kuliko kuwemo ndani ya serikali wakichukuwa mishahara yao na zaidi ya watu 20 wengine wa ziada. Kwa hivyo mnapotuletea makala na tasmini pumba kama hizi lazima mkumbuke wakati wa kudanganywa kwa watanzania umekwisha wanachokiamini ni kile wanachokiona kwa macho live muheshimiwa raisi akitumbua majibu. Kwa mwezi mamlaka ya mapato inakusanya trillion na zaidi hapo muheshimiwa raisi hata kazi hajaanza we acha tu. Ngoja ateuwe wakurugenzi, wakuu wa mikoa na wilaya. Vile vile kwenye vikosi vya ulizi na usalama wa raia atakapomaliza Tanzania itakuwa nchi ya heshima Africa na duniani kwa ujumla ingawaje hivi sasa tayari heshima hiyo imeshaanza kujengekeka duniani kote. Tumuombee raisi wetu afanikiwe na hii vita ya mafisadi kwani wapo mafisadi hata katika mitandao ya kijamii na tukiwashtukia basi tusichelewe kuwatumbua majibu.

    ReplyDelete
  2. Kuna habari a sifa nyingi za uzushi anapewa nyerere baada ya kufariki nyerere ndio alianzisha kuteua watu ovyo bila ya kujali walichokisomea yeye ndio alikuwa na serikali ya mambumbu yeye ndio alikuwa anawaamisha watu sio kuwafukuza ni mawazir wangapi wamefukuzwa na nyerere?

    ReplyDelete
  3. kuna watu hawataki kukubali kuwa Magufuli ndio rais wao na Lowasa yuko monduli anachunga
    mwacheni Magufuli afanye kazi yake afu mnajua kutoa mada tuu na kejeli kibao kwa Magufuli urais ni kazi ngumu na anachofanya jamaa ni cha kupongezwa
    baada ya kumkejeli tutumie nguvu zetu kumsapot ili kila mtanzania anufaike na rasilimali za nchi hii
    kusimamishwa kwa watumishi na kupokea mshahara wakiwa nje ni bora kuliko uwaache waendelee kujichotea tuu mapesa
    we mtoa mada hujielewi na sio mchambuzi unakurupuka tuu wala takwimu kamili huna zzaidi ya ushabiki mandazi tuu wakijinga
    ila sishangai ndo maana ya udaku

    ReplyDelete
  4. Bora atokomee kuliko aendelee kuwepo kazini na kuliletea Taifa hasara kwa wizi wake na ulafi uliokithiri. Wizi wanaoufanya ni mkubwa. Bora wawe chonjo wasubiri hiyo nusu mshahara kuliko kutuibia taifa zima. Nusu mshahara hauwezi jenga mahekalu. Sana sana hela ya mlo. Hawatufai bora mueshimiwa aendeleee kuwasambalatisha tu. Bila hivyo maendeleo hayatakuwepo kwenye hizi nchi zetu za bara hili la Afrika

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad