Jumba la Mchungaji Mama Rwakatare, Hoteli za Double Tree na Slip Way Kubomolewa

Wakati operesheni ya kuweka alama ya X kwenye nyumba zilizojengwa mabondeni, maeneo ya wazi na kinyume na taratibu ikiendelea, Hoteli za Double Tree na Slip Way nazo zimekumbwa na pigo hilo.

Hoteli hizo pamoja na nyumba ya Maheshbhai Patel na baadhi ya wamiliki wengine wa nyumba ambao kuta zake zimejengwa karibu na barabara ya Slip Way eneo la Msasani Peninsula, wamepewa siku saba kuzibomoa.

Jana, uongozi wa Manispaa ya Kinondoni uliweka alama za X na kuwaonya wamiliki hao kwamba, wasipobomoa manispaa itazibomoa na kudai gharama za ubomoaji.

Akizungumza kwa simu jana, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi alisema Serikali haitaurudi nyuma katika kutekeleza sheria hata kama kuna watu wana jeuri ya pesa.

Alisema Manispaa ya Kinondoni iliwapatia vibali vya kupendezesha maeneo ya pembezoni mwa barabara ikiwamo kupanda maua, lakini wao badala ya kutimiza masharti ya vibali walizungushia kuta jambo ambalo hawatalivumilia.

Wangependezesha na kufunga minyonyoro kuzuia kuharibiwa mazingira yao kama walihisi wananchi wangeharibu, lakini siyo kujenga kuta.

“Nimewaagiza Kinondoni wawapatie notisi ya siku saba kubomoa kwa hiari. Wasisubiri Serikali ivunje.

"Tutabomoa hadi lile jengo lililopo karibu na Hospitali ya Ami lililovunja sheria, yule hawezi kuonyesha jeuri ya fedha,” alisema Lukuvi.

Alisema Serikali ina mpango maalumu wa kubomoa majengo yote yaliyojengwa kinyume na sheria Masaki na Oysterbay na wameanza na Barabara ya Slip Way.

Katika hatua nyingine, sakata la bomoabomoa pia limewakumba waliojenga katika hifadhi za mikoko baada ya watumishi wa Baraza la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) na maofisa misitu wa Manispaa ya Kinondoni kuweka alama ‘X’ katika nyumba zaidi ya 30 ikiwamo ya kiongozi wa Kanisa la Mikocheni B Assemblies of God, Dk Getrude Rwakatare.

Kazi hiyo ilianza jana mchana katika maeneo mbalimbali ya Dar es Salaam ikiwamo, katika Mtaa wa Ally Sykes, Kawe na Jangwani Beach eneo la Mbezi Beach. Ofisa Misitu Msaidizi wa Manispaa ya Kinondoni, Issa Juma aliwaambia wanahabari kuwa kazi hiyo ni endelevu.
Tags

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hapa kazi tu naona hata jengo la tanesco ubungo lililoleta utata miaka ya nyuma linaweza kukubwa nalo au? Kazi kweli kweli, mimi naomba msamaha jamani maana hii ni kilio wala sio huzuni tena tupeni hata mwaka mmoja basi maana nyumba zingine tumejenga kwa miaka 30 hadi kumalizika. mshahara wangu ni 110,000/- je nikibomoa naweza kujenga tena umri wangu ni miaka 50 sasa

    ReplyDelete
  2. Kwanza kabisa napenda kuanzia na kusema maeneo mengi ya wazi nchini yalivamiwa kwa baraka za CCM
    Wanainchi walianza na kufunguwa matawi ya wakelekwetwa wa CCM viongozi wakuu wa ccm walifunguwa matawi haya kwa vishindo
    Watu wa kaanza kujenga sehemu hizi hasa Jangwani Dar , yakawa ni mazoea mafuriko yakitokea missada inatoka serikali ya ccm ikawa inatumia mabilion ya fedha , Tanzania tuna sehem kubwa sana ya watu kuuishi sasa kwanini wasitengeze maandalizi kwa watu hawa?
    Kabla , Kama ni uvamizi ccm ni namba moja maeneo mangapi nchini yalikuwa wazi CCM imejenga ofisi zao.
    Nafikiriki hata hayo mahekalu ni kulipiza kisasi tu ,
    Yatawagharimu sana haya ccm
    Vibali na hati si mlitoa wenyewe
    Kisiwe kisingizio wamejenga kwenye maeneo
    Hata ughaibuni mafuriko yako tafuteni jinsi gani ya kuepuka na kuyazuia
    Hali ya hewa na mabadiliko yapo dunia nzima msilete wivu na ujinga wa kufikiri nyinyi viongozi wa serikali ya ccm

    ReplyDelete
  3. BORA WATOZWA PESA KWA MAKOSA WALIYOYAFANYA KULIKO KUVUNJIWA MAJUMBA YAO.HUO NI UMASKINI WA KULAZIMISHWA.SHERIA ILIKUWA WAPI WAKATI WANAWEKA MSINGI WA NYUMBA HIZO?

    ReplyDelete
  4. WAKATI MWINGINE NI CHUKI ZA KIBINAFSI.KWANI SHERIA ILIKUWA WAPI WAKIWEKA JIWE LA MSINGI.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad