Kajala Adaiwa Kunasa Ujauzito wa Kigogo

Good news? Huenda mambo yanaweza yakawa yamejipa kwa mwigizaji Kajala Masanja ‘Kay’ kwani kuna taarifa zinadai kuwa mwigizaji huyo amenasa mimba ya kigogo serikalini.

Chanzo makini kilicho karibu na staa huyo ambaye ana mtoto mmoja aliyezaa na prodyuza mkongwe Bongo, Paul Matthysse ‘P Funk’ (Paula), kimepenyeza ubuyu huo kuwa Kajala ana mimba ya zaidi ya miezi mitano na amegusiwa kuwa ni ya kigogo serikalini ambaye hataki kumtaja jina.

“Hivi hamna habari? Kajala mbona mjamzito. Tena yeye alianza kunasa kabla hata ya Wema, nashangaa mnakomalia kuripoti mimba ya Wema tu, Kay mmemuacha na kigogo wake,” kilimwaga ubuyu chanzo hicho.

Baada ya kupewa ubuyu huo, juzi Alhamisi, mwanahabari wetu wakati anaanza kuichimba habari hiyo, alitembelea kwenye ukurasa wa Instangram wa Kajala na kukutana na ujumbe ulionesha dhahiri kuwa mwigizaji huyo anajiandaa kuitwa mama kwa mara nyingine.

“Hey IG…do me a favor…help me to choose a name of my new baby coz Pau wants a name with P in the beginning and mimi sitaki..” aliandika Kajala akiwataka wafuasi wake katika mtandao huo wamsaidie kuchagua jina la mtoto wake ajaye kwani Pau (Paula) anataka jina linaloanza na herufi P lakini yeye hataki.

Alipopigiwa simu na mwanahabari wetu kuhusiana na ujumbe huo sanjari na taarifa za kuwa ni mjamzito wakati gazeti hili linakwenda mitamboni, Kajala alikata simu. (Huenda alikuwa sehemu ambayo hakuweza kuzungumza, bila shaka ataona habari hii na kutoa ufafanuzi zaidi kwani ni jambo la heri.)

Chanzo: GPL

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Yaani nanyie mnakera hii nayo ni habari kwani mimba ni kitu cha ajabu au yeye ni nani, mbona kuna habari nyingi za maana kwamfano watu kuhamishwa mabondeni nk

    ReplyDelete
  2. hizi mimba mwaka huuuu
    hehehe kisa tiffany
    kila malaya ana mimba
    fyuuuuuuuuuu

    ReplyDelete
  3. Upuuzi mtupu,mmekosa newz?

    ReplyDelete
  4. Hamna hadhi kabisa ya kujiita waandishi wa habari yaani ni zero no wonder waziri muhusika ameyafungia magazeti radio na tv shauri kiukweli nyinyi mnajiita eti ni waandishi or whatever the fuck you call yourselves ni wazushi fitina vizabizabina wachonganishi mna roho za kutu kuna siku mtakuja kulia kilio cha mbweha mdomo juu kudadeki zenu i hate you all fake journalists

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad