Kinana Ataka Wabunge CCM Wafuate Moto wa Ukawa

Wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wamefunguliwa milango na chama chao kuhakikisha wanaibana serikali itekeleze ilani na kuziba mianya ya ubadhirifu wa fedha za umma.

Hatua hiyo imelenga kuhakikisha kwamba wapinzani wanakosa hoja za kuidhoofisha serikali bungeni.

Wabunge wa vyama vya upinzani wamekuwa wakiibana serikali kwa kuikosoa na kufichua mianya yote ya ufisadi inayofanywa viongozi mbalimbali waliopo madarakani.

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, ndiye aliyetoa rungu hilo katika semina ya siku mbili ya wabunge wa chama hicho iliyofanyika Makao Makuu ya CCM mjini hapa jana.

Kikao hicho kilianza juzi chini ya Kinana, na kwa siku ya kwanza kinadaiwa kilikuwa na ajenda tatu; wajibu wa wabunge wa CCM kwa serikali, tathmini ya uchaguzi mkuu na mchakato wa kura za maoni ndani ya Chama, huku siku ya pili ambayo ni jana kulikuwa na ajenda moja ya Ilani ya chama hicho na namna ya kuitekeleza.

Mbali na hilo, Kinana aliwataka wabunge kuhakikisha wanapambana ili sheria zote kandamizi kwa wananchi zifutwe, jambo litakalowawekea wananchi mazingira mazuri.

Hata hivyo, katika ajenda ya wajibu wa wabunge wa CCM kwa serikali kwenye mfumo wa vyama vingi, iliwasilishwa na aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Pius Msekwa, ambayo ilibainisha namna ambavyo kambi ya upinzani bungeni ilivyo na mkakati wa kuidhoofisha serikali ili katika uchaguzi wao wachukue madaraka.

Katika mada hiyo, Msekwa aliwataka wabunge wa CCM kutafuta mbinu za kujilinda na kujitetea ili wapinzani wakose hoja za kuidhoofisha serikali.

"Wajibu wa kila mbunge wa CCM ni kuiwezesha serikali ya chama chake kutekeleza majukumu yaliyoahidiwa katika ilani ya uchaguzi kwa kupitisha miswada ya sheria inayowasilishwa na serikali kwa madhumuni hayo, ikiwamo bajeti zinazopendekezwa na serikali," ilieleza sehemu ya mada hiyo iliyowasilishwa na Msekwa.

Aidha, Msekwa alisema ni halali kabisa kwa wabunge wa CCM kutumia wingi wao kuidhinisha maombi ya bajeti yanayopelekwa bungeni na serikali ili kuiwezesha kutimiza ahadi zilizotolewa kwa wananchi kupitia ilani ya uchaguzi ya Chama.

Kwa upande wa Kinana, aliwataka wabunge hao 'kufinya' hoja ili isiwe kazi ya wapinzani kuchokonoa moto, jambo litakalowafanya kukosa mwanya wa kuilipua serikali.

"Katibu Mkuu katutaka tufanye kazi kama wabunge, tutetee na wananchi na amesema hakuna kamati kuu iliyoagiza wabunge wasiibane serikali, hasa Kinana anachotaka ni nchi hii kufanikiwa kwa kuziba mianya yote ya ubadhirifu wa fedha za umma na kutatua matatizo yanayowakabili wananchi ili wapinzani wakose hoja," walisema baadhi ya wabunge katika semina hiyo.

Kuhusu kufuta kodi ambazo ni mzigo kwa wananchi, wabunge hao wamejadili na kukubaliana  namna ya kuhakikisha wanaondoa kodi mzigo ambazo ni kero kwa wananchi na kandamizi.

Inadaiwa miongoni mwa kodi ambazo ni mzigo kwa wananchi ni kodi ya Ewura ambayo ina kodi ya ukaguzi, uthibiti ambazo ni   kitu kimoja, hivyo zitachambuliwa na kufutwa ili kuleta unafuu kwa wananchi, hivyo kusaidia hata bei ya mafuta kushuka.

Hata hivyo, wakichangia mijadala baadhi ya wabunge wametaka kuwapo na bandari ya nchi kavu mkoani Dodoma kwa kuwa ni mkoa wa kati ambao ni rahisi kwa kila sehemu kuchukulia mizigo yake hata nchi za jirani.

Aidha, wabunge wengi wametaka upatikanaji wa maji mijini na vijijini huku wengi wakisema yasipopatikana itakuwa ni hati hati kwa CCM kushinda uchaguzi ujao kwa hofu ya kusulubiwa na wapigakura wanawake ambao hiyo ndiyo kero yao kubwa.

Kuhusu sheria kandamizi, Kinana aliwaambia wabunge hao kuwa sheria zingine za mkoloni mpaka sasa zipo na kwamba hazimsaidii mwananchi wa kawaida.

Kadhalika katika kikao hicho Kinana alisema vyombo vya habari vinapendwa lakini wabunge hao wajitahidi kutunga sheria hasa itakayotetea maslahi kwa waandishi wa habari.

"Katibu Mkuu anasema ikiwekwa sheria ya aina hiyo, waandishi kulipwa vizuri hasa kwenye vyombo binafsi, magazeti mengine yatakufa yenyewe huna haja ya kugombana nayo, maana mwandishi anatakiwa aajiriwe na apate haki zake...hii itafanya kusiwe na uholela holela wa kusajili magazeti wakati mmiliki hana uwezo wa kuajiri na matokeo yake utakuta gazeti habari zake nyingi na mwandishi wetu," alisema mmoja wa wabunge ambaye aliomba hifadhi ya jina lake.

Alipotakiwa kuzungumzia kuhusu semina hiyo, Katibu wa Wabunge wa CCM, Jenista Mhagama, alisema hataweza kuzungumzia chochote kwa kuwa semina hiyo imeratibiwa na chama hivyo anayetakiwa kuzungumza ni Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye.

Kwa upande wake. Nnauye alisema: "Hatujatoa taarifa kwa umma juu ya semina na hatujawaambia lolote.
Tags

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. koma wewe kinana twambie meno ya tembo zurich
    mbona husemi mawaziri mizigo au mzigo alikuwa kikwete
    fyuuuuuuuuu
    cmm au shoga yako nape kapata uwaziri kwa midomo yenu

    ReplyDelete
    Replies
    1. Taratibu bana, unatutemea mate....eboh!!
      Kama umeumia saaaaana saga chupa ubwie.......HAPA KAZI TU!!

      Delete
    2. kuna mijitu shida kweli apa dunia sasa apo nape anakujaje au unawashwa unataka nape akuchomeke nao
      kubwa jinga wew icho cha maana ulichoona umeandika kweli wewe muuimba tarabu nenda kwa mzee yusuph akuajiri
      ndo shida ya kufanya kazi saloon
      shoga wewe
      hapa kazi tuu

      Delete

  2. AnonymousJanuary 20, 2016 at 2:33 PM
    koma tena tena koma wacha tuseme

    meno ya tembo zurich kimya tumeisha watuma wabunge bungeni
    na bomoabomoa
    ya zanzinbar mbona mmefyata
    bi asha yupo wapi akhera na domo lake

    ReplyDelete
  3. ukitaka mazishi ya kitaifa lazima uwe ccm
    sina kinyongo na marehemu
    lakini kama angekuwa cmm jeneza lingekuwa na bendera ya taifa
    huyu hakuwa kiongozi wa kitaifa tusitumie bendera only kwa watu fulani
    zanzibar wanasota leo RIP kisa karudi ccm na alikuwa mgonjwa miaka mingi
    na mlimwabia ccm lazima arudi ccm ili mazishi yake yawe ya kitaifa
    fuck u cmm

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad