Kipya Kinachoendelea Kuhusu Kuanzishwa Kwa Mahakama ya Mafisadi Tanzania

SERIKALI imewahakikishia Watanzania kuwa mchakato wa kuanzishwa kwa Mahakama Maalumu ya mafisadi na wezi, umefikia hatua nzuri. Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Harrison Mwakyembe alisema hayo juzi bungeni mjini hapa, wakati akichangia Hotuba ya Rais ya Ufunguzi wa Bunge.

Akizungumzia mchakato wa kuanzishwa kwa mahakama hiyo maalumu, Mwakyembe alisema unakwenda vizuri na utakapokamilika Watanzania watafahamishwa. “Kiongozi wa Serikali ya Awamu ya Tano, akitoa tamko lazima litekelezwe.mwakyembe (1)

Kama tunakumbuka Rais, kwa nyakati tofauti kipindi cha kampeni, aliahidi kuanzisha Mahakama Maalumu ya Mafisadi na Wezi,” alisema Mwakyembe. Akiizungumzia hotuba ya Rais, Mwakyembe alisema ikiachwa hotuba ya Mwalimu Nyerere, ya Magufuli pia ni bora na iligusa mioyo ya Watanzania wenye nia njema na Taifa.

“Wakati rais anatoa hotuba yake iliyokuwa na aya 160, alipigiwa makofi na vigelegele mara 137, ni zaidi ya asilimia 86, ya Dk Martin Luther ambaye ni Mmarekani mweusi,” alisema na kuongeza kuwa hatua hiyo, imewaweka pabaya wapinzani waliokuwa wanapinga kila kitu.

Dk Mwakyembe alisema tatizo ni kwamba kwa hotuba hiyo, yeyote akijaribu kuipinga, wananchi watamuona wa hovyo. Aliendelea kusema; “Wamejaribu (upinzani) kutoka kwenye mjadala, kwa hoja tu ya TBC (Shirika la Utangazaji Tanzania), ili wasiwepo kwenye mjadala, kwani wakiwepo lazima wataisifia tu.”
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. mafisadi ni nyinyi wenyewe mliopeana wadhifa hiyo mahakama mtamshitaki nani? wewe maembe na wenzio ndo mlistahili kushtakiwa, au mahakama ya lowasa na samweli sita.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad