Kulihitajika Uchunguzi wa Kina Dhidi ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza Dr. Faisal Kwanza Kabla ya Kufukuzwa

Ukweli ni kuwa kufukuzwa kazi kwa aliyekuwa katibu tawala wa mkoa wa Mwanza Dr. Faisal kumeambatana na ukiukwaji mkubwa wa maadali ya utumishi wa umma! Dr. Faisal amefukuzwa kazi kwa kuegemea ushahidi wa upande mmoja huku chanzo cha kufukuzwa kwake kikiwa hakijawekwa bayana! Hili ni tatizo kubwa! 

Tunaambiwa kuwa rais Magufuli alichukuwa uamuzi wa kumfukuza kazi mtumishi huyo wa umma muda mfupi sana baada ya kupokea simu kutoka kwa mkuu wa mkoa wa Mwanza ndugu Magesa Mlongo! 

Kimsingi rais alitakiwa kupima kwa kina aina ya mtu anayempa maelezo! Magesa Mlongo !mashitaka yake kwa rais yalitakiwa kupimwa kwa umakini mkubwa! Kulitkiwa subira na uchunguzi wa kina hasa ikizingatiwa historia aliyo nayo ndugu Mlongo!

Tungependa kuona haki inatendeka na utu unalindwa dhidi ya hili!

By G Sam From Jamii Forums

Tags

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Uchunguzi wa kina kivipiiiii........haya mambo ya uchunguzi wa kina ndio yameifikisha hiyo Nchi mahali ilipo. Huyu jamaa kafanya makosa ni haki ya mwajiri wake kumwajibisha mara moja ili kuokoa muda na Wananchi waendelee na maendeleo yao. Huo muda wa kufanya uchunguzi utapatikana wapi na nani atagharamia hizo gharama za uchunguzi. Ni jukumu la kila mtumishi wa umma kuwajibika kwa nidhamu ya hali ya juu, na sio kusubiri mpaka siku atumbuliwe ndio aje na visingizio chungu mzima. Na pia mwandishi wa hiyo habari acha uongo wako wa mchana kweupe
    "Tunaambiwa kuwa rais Magufuli alichukuwa uamuzi wa kumfukuza kazi mtumishi huyo wa umma muda mfupi sana baada ya kupokea simu kutoka kwa mkuu wa mkoa wa Mwanza ndugu Magesa Mlongo!" .......huo ni uongo na pia ni uzushi wa hali ya juu wa huyo mwandishi. Huyo jamaa alitumbuliwa kwa sababu ya kuonyesha utovu wa hali ya juu wa nidhamu katika kikao cha usalama cha mkoa. Tafadhalini acheni majungu hayatawasaidia chochote #HAPAKAZITU

    ReplyDelete
  2. Hakuna cha uchunguzi wala upelelezi ukiaribu unakwendaa

    ReplyDelete
  3. Ni kweli Muheshimiwa Rais hembu ktk hili fanya uchunguzi mwenye shida hapa ni aloshtaki siku zote wanakimbilia kushtaki ndo wana matatizo

    ReplyDelete
  4. Check and balance ni muhimu kwa nchi zetu changa usikute kuna matatizo ya kiuongozi, au kiutawala.Mungu ibariki Tanzania.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad